Pata taarifa kuu

Mzozo wa Sudan waatishia kuenea na kuzitia wasiwasi nchi jirani

Nchi saba jirani za Sudan zimedai katika mkutano wa kilele Alhamisi nchini Misri msaada wa wafadhili wa kimataifa kwa minajili ya kuwapokea zaidi ya wakimbizi 700,000 waliotoroka nchi hiyo kutokana na vita vinavyoendelea, ambapo miili 87 iligunduliwa katika kaburi la pamoja, kulingana na Umoja wa Mataifa.

Cairo imeandaa mkutano na nchi saba jirani na Sudan.
Cairo imeandaa mkutano na nchi saba jirani na Sudan. Β© AFP
Matangazo ya kibiashara

Katika mipaka ya Pembe ya Afrika, Sahel na Mashariki ya Kati, Sudan imetumbukia katika machafuko tangu Aprili 15, majenerali wawili walioingia madarakani kwa kutumia silaha kila mmoja amemgeukia mwenzake. Tangu wakati huo, mapigano kati ya jeshi la Jenerali Abdel Fattah al-Burhane na wanamgambo wa Kikosi cha Msaada wa Haraka cha Jenerali Mohamed Hamdane Daglo (FSR) yamesababisha vifo vya watu 3,000 na zaidi ya milioni tatu kuyahama makazi yao na wengie kuwa wakimbizi wa ndani.

Misri, nchi jirani yenye ushawishi mkubwa upande wa kaskazini, imepokea idadi kubwa ya wakimbizi zaidi ya 255,000, ikifuatiwa na Chad (240,000) na Sudan Kusini (160,000). Jumuiya ya kimataifa, ambayo iliahidi dola bilioni 1.5 katika mkutano wa kilele mwezi Juni, "lazima itimize ahadi" na "kusaidia nchi jirani", amesisitiza rais wa Misri Abdel Fattah al-Sissi.

'Kusambaa kwa Silaha'

"Katika wiki moja, tumepokea zaidi ya watu 150,000, wengi wao wakiwa wanawake na watoto" wakikimbia Darfur, ambako ukatili mbaya zaidi umerekodiwa, ameongeza rais wa Chad, Jenerali Mahamat Idriss DΓ©by Itno.

Wakati huo huo siku ya Alhamisi, Ofisi ya Haki za Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa imeripoti kwamba takriban watu 87 waliouawa na RSF na washirika wao wamezikwa katika kaburi la pamoja huko Darfur ambako Umoja wa Mataifa ulikuwa tayari unazungumzia uwezekano wa "uhalifu dhidi ya ubinadamu" katika mzozo wa sasa wa kikabila. .

Akisikitishwa na "kupanda kwa bei" na "uhaba" katika mikoa ya mpakani, rais wa Afrika ya Kati Faustin Archange TouadΓ©ra, ameonya dhidi ya kuongezeka kwa "mzunguko wa silaha ndogo ndogo katika mipaka ya Sudan". Nchi hizo saba zilizokusanyika mjini Cairo, pamoja na wakuu wa Umoja wa Afrika na Umoja wa Nchi za Kiarabu, zimesisitiza kwamba zitafanya kila waliwezalo kuzuia Sudan kuwa "El Dorado kwa ugaidi na uhalifu uliopangwa", kulingana na taarifa yao kwa vyombo vya habari.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.