Pata taarifa kuu

Uchaguzi wa urais nchini Gabon: Rais Ali Bongo atangaza kuwania muhula wa tatu

Rais wa Gabon, Ali Bongo Ondimba, mwenye umri wa miaka 64 na aliyeko madarakani kwa takriban miaka 14, ametangaza siku ya Jumapili, Julai 9, kwamba atakuwa mgombea kwa muhula wa tatu katika uchaguzi wa urais ambao umebangwa kufanyika Agosti 26. 

Rais wa Gabon, Ali Bongo Ondimba.
Rais wa Gabon, Ali Bongo Ondimba. AFP - LUDOVIC MARIN
Matangazo ya kibiashara

"Ninatangaza rasmi leo kuwa mimi ni mgombea" katika uchaguzi wa urais, amesema mbele ya umati wa wafuasi katika hotuba, iliyorushwa moja kwa moja kwenye ukurasa wake wa Facebook. Ameyasema hayo katika Ukanda Maalum wa Kiuchumi (SEZ) wa Nkok, karibu na mji mkuu Libreville.

Wakati huo huo Alexandre Barro Chambrier, mmoja wa vigogo wa upinzani, ameteuliwa siku ya Jumapili mchana kuwakilisha chama chake katika uchaguzi wa Agosti 26. Chama cha RPM kimekutana katika kongamano lisilo la kawaida na wamemteua hivi punde. Ni lazima mkutano uandaliwe mchana ili kutangaza ugombea huu kwa wafuasi wake. 

Alexandre Barro Chambrier ambaye ni Mwanauchumi na mbunge kwa muongo mmoja, alikuwa waziri mara kadhaa chini ya utawala wa Omar Bongo na kisha wakati wa mamlaka ya Ali Bongo ambapo alikuwa waziri mwenye dhamana ya Mafuta. Aliingia upinzani mwaka 2016.

Serikali ya Gabon ilitangaza Jumanne kuwa uchaguzi wa rais, wabunge na serikali za mitaa utafanyika tarehe 26 Agosti. Rais anayeondoka Ali Bongo Ondimba, ambaye familia yake imetawala nchi hii ndogo ya mafuta kwa zaidi ya nusu karne, anapewa nafasi kubwa ya kushinda muhula wa tatu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.