Pata taarifa kuu

Gabon :Uchaguzi Mkuu kufanyika Agosti

Gabon itaanda uchaguzi wake wa urais pamoja na ule wa wabunge tarehe 26 ya mwezi Agosti mwaka huu kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa serikali katika taifa hilo la Afrika Magharibi.

Gabon itaanda uchaguzi wake mkuu mwezi Agosti mwaka huu
Gabon itaanda uchaguzi wake mkuu mwezi Agosti mwaka huu AFP - ISABEL INFANTES
Matangazo ya kibiashara

Rais Ali Bongo Ondimba hajasema iwapo atawania katika uchaguzi huo japokuwa kuna asilimia kubwa ya uwezekano wa kutangaza kugombea tena.

Chama chake chenye nguvu cha Gabon Democratic Party (PDG) kina wabunge wengi wenye nguvu katika mabunge yote mawili na kinashinikiza rais atangaze kuwa atawania tena.

Mnamo 2009, Bongo mwenye umri wa miaka 64 alichukua hatamu kutoka kwa babake Omar Bongo Ondimba, mtawala wa nchi hiyo yenye utajiri wa mafuta kwa kipindi cha miaka 41.

Alitangazwa mshindi wa uchaguzi mkuu wa mwaka wa  2016, uchaguzi ambao ulikuwa na ushindani mkubwa ambapo alimshinda mpizani wake wa karibu Jean Ping kwa kura 5,500. Jean Ping,alidai uchaguzi huo uligubikiwa na udaganyifu na haukufanywa kwa uwazi.  

Bongo alipatwa na ugonjwa wa kiharusi mwaka wa 2018 hali iliyomlazimu kujiondoa kwenye ulingo wa kisiasa akipokea matibabu, hali ambayo upinzani ulihoji uwezo wake wa kuongoza nchi.

Familia ya Bongo imeongoza taifa hilo kwa kipindi cha miaka 55 hatua ambayo imekashifiwa na wapinzani.

Licha ya upinzani kukashifu uongozi wa Bongo, umeshindwa kukubaliana kuhusu uteuzi wa mgombea mmoja kuwania urais ambapo wagombea 15 wa upinzani wametangaza nia yao ya kugombea.

Mwezi Aprili, bunge nchini Gabon lilipiga kura kutekeleza mageuzi kwenye katiba kupunguza muhula wa rais kuongoza kutoka miaka saba hadi miaka mitano.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.