Pata taarifa kuu
UCHAGUZI-SIASA

Uchaguzi wa urais: Muhula wa rais wapunguzwa kutoka miaka 7 hadi 5 na duru mbili hadi moja

Bunge la Gabon lilipiga kura Alhamisi kuhusu marekebisho ya Katiba na kupunguza kutoka miaka 7 hadi 5 muhula wa rais wa Jamhuri na duru mbili hadi moja, ikiwa imesalia miezi 5kabla ya uchaguzi wa rais na wa wabunge.

Rais wa Gabon Ali Bongo ahutubia wabunge wa nchi yake katika makao makuu ya Bunge mnamo Juni 2021.
Rais wa Gabon Ali Bongo ahutubia wabunge wa nchi yake katika makao makuu ya Bunge mnamo Juni 2021. AFP - WEYL LAURENT
Matangazo ya kibiashara

Mabadiliko haya, hasa kura ya duru moja, yamelaaniwa na upinzani (ambao kwa sasa umegawanyika) ukibini kwamba ni njia ya "kuwezesha Ali Bongo Ondimba, ambaye ametawala nchi hiyo kwa zaidi ya miaka 13, kurudi kuchaguliwa tena. Waziri Mkuu Alain-Claude Bilie-By-Nze amekaribisha mara moja marekebisho haya, "matokeo ya maafikiano yaliyotokana na mashauriano ya kisiasa ya siku 10" mwezi Februari "kati ya wengi na upinzani".

Bunge la Kitaifa na Seneti, zilizokutana huko Libreville, "zilipitisha rasimu ya marekebisho ya Katiba", kwa "86% ya kura zilizopigwa", "ikiwa ni kura nyingi zilizohitajika ya theluthi mbili", alitangaza Spika wa Baraza la Bunge la Kitaifa, Faustin Boukoubi, baada ya kura iliyotangazwa moja kwa moja kwenye televisheni ya umma ya Gabon Première.

Hata hivyo, mazungumzo haya yalikuwa yalisusiwa na viongozi muhimu wa upinzani na vyama vyao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.