Pata taarifa kuu
USALAMA-HAKI

Misri yamhukumu mwanamume aliyepatikana na hatia ya kuua wanawake

Mwanamume mmoja ameuawa siku ya Jumatano baada ya kupatikana na hatia ya kumuua mwanafunzi ambaye alikataa kupokea mahari yake, mauaji ambayo yalizua ghadhabu nchini Misri, mamlaka imesema.

Misri ilitekeleza idadi ya nne ya watu walionyongwa duniani mwaka 2022, kulingana na shirikala kimataifa la Amnesty International.
Misri ilitekeleza idadi ya nne ya watu walionyongwa duniani mwaka 2022, kulingana na shirikala kimataifa la Amnesty International. AFP
Matangazo ya kibiashara

Mamlaka ya magereza ya Misri "imetekeleza hukumu ya kifo dhidi ya Mohamed Adel", mamlaka imesema, katika taarifa iliyorushwa na vyombo vya habari vya serikali. Alihukumiwa mnamo mwezi Juni 2022 kwa "mauaji ya kukusudia" ya Nayera Achraf, ambaye alikuwa akisoma katika chuo kikuu kimoja naye, mamlaka imeongeza.

Kesi hii iliyotangazwa sana ilifanyika baada ya kifo cha mwanafunzi huyo aliyechomwa kisu huko Mansoura, mji ulioko kilomita 130 kaskazini mwa Cairo. Mauaji yake yalirekodiwa na video ilisambazwa sana mtandaoni.

Muda mfupi kabla ya kuuawa kwake, Nayera Achraf alisema alihofia maisha yake na aliwasilisha malalamiko kwa mamlaka. Wakati wa kesi hiyo, upande wa mashtaka ulionyesha jumbe kutoka kwa Mohamed Adel, ambapo alitishia "kumkata koo". Ni nadra sana, kesi ya Bw. Adel ilirekodiwa na kutangazwa moja kwa moja na baadhi ya vyombo vya habari, kukiwa na wazo, kulingana na mahakama, la "kuwazuia watu wengi zaidi" kufanya uhalifu kama huo.

Kesi hiyo ilizua mjadala nje ya Misri kwa sababu siku chache baada ya Nayera Achraf, mwanafunzi wa Jordan aliuawa kwa kupigwa risasi huko Amman, pengine kwa sababu hizo hizo. Kisha, mwezi Agosti, mwanafunzi wa uandishi wa habari aliuawa kwa kuchomwa kisu huko Zagazig, kilomita 60 kaskazini mwa Cairo.

Katika nchi ambayo Uislamu mkali umezidi kuimarika tangu miaka ya 1970, uchunguzi uliofanywa na Umoja wa Mataifa mwaka 2015 ulihesabu karibu wanawake milioni nane waathiriwa wa unyanyasaji na waume zao, ndugu au mgeni katika maeeo ya umma. Misri ilitekeleza idadi ya nne ya watu walionyongwa duniani mwaka 2022, kulingana na shirikala kimataifa la Amnesty International.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.