Pata taarifa kuu
USHIRIKIANO-DIPLOMASIA

Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri kufanya ziara ya kihistoria Syria na Uturuki

Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri, Sameh Choukri, anaanza Jumatatu hii, Februari 27, ziara ambayo itampeleka Damascus, Syria, kisha nchini Uturuki. Nchi mbili ambazo Misri ilikuwa na uhusiano mbaya na ambayo inataka kuonysha msaada wake na udugu wake baada ya tetemeko la ardhi, Wizara ya Mambo ya nje huko Cairo imesema.

Waziri wa Mambo ya nje wa Misri, Sameh Choukri, wakati wa kikao cha kawaida cha 36 cha Bunge la Umoja wa Afrika (AU), katika makao makuu ya umoja huo huko Addis Ababa, mnamo Februari 19, 2023.
Waziri wa Mambo ya nje wa Misri, Sameh Choukri, wakati wa kikao cha kawaida cha 36 cha Bunge la Umoja wa Afrika (AU), katika makao makuu ya umoja huo huko Addis Ababa, mnamo Februari 19, 2023. AFP - AMANUEL SILESHI
Matangazo ya kibiashara

Mahusiano ya Misri na Syria yalivunjwa mnamo 2013 na Rais Mohamed Morsi, ambaye alifikia hata kutaja uwezekano wa kupeleka wanajihadi kupigana dhidi ya serikali ya Bashar al-Assad.

Tangu wakati huo, uhusiano ulivunjika na kusalia hivyo. Hii haikuzuia Misri kutuma misaada ya kibinadamu na kupeleka timu za uokoaji kwenda Damascus.

Cairo imefanya vivyo hivyo na Uturuki. Uturuki ambayo uhusiano wa kidiplomasia haukuvunjika, lakini ulipungua, kwa sababu ya Akara uunga mkono vuguvugu la Udugu wa Waislamu "Muslim Brotherhood".

Mahusiano ambayo yameanza kurejea polepole tangu marais Sissi na Erdogan walikutana wakati wa michuano ya Kombe la Dunia la Soka huko Qatar na, hivi karibuni, Uturuki ilimfukuza mwandishi wa habari kutoka vuguvugu la Udugu wa Waislamu ambaye alikuwa akiongoza kampeni dhidi ya serikali ya Misri kupitia kituo cha runinga kutoka Istanbul.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.