Pata taarifa kuu
GABON-SIASA

Gabon yampata waziri mkuu mpya, Rose Christiane Raponda

Kwa mara ya kwanza katika historia, rais wa Gabon, Ali Bongo, amemteua mwanamke, Christiane Ossouka Raponda kuhudumu kama waziri mkuu katika serikali. Ni mwanamke wa kwanza kuteuliwa kwenye nafasi hiyoi, miaka 60 baada ya uhuru wa nchi hiyo.

Rose Christiane Ossouka Raponda, ilikuwa Oktoba 6, 2018, wakati alikuwa meya wa Libreville.
Rose Christiane Ossouka Raponda, ilikuwa Oktoba 6, 2018, wakati alikuwa meya wa Libreville. Joel TATOU / AFP
Matangazo ya kibiashara

Rose Christiane Ossouka Raponda, 56, sio maarufu nchini Gabon. Rose Christiane Ossouka Raponda, ambaye ni mwanamke wa kwanza kuteuliwa kama Waziri Mkuu, pia alikuwa mawanamke wa kwanza kuchaguliwa kuwa meya wa mji wa Libreville mnamo mwaka 2014.

Hata hivyo mwaka 2019, Rais Ali Bongo alimtenguwa kwenye wadhifa wake na kumteuwa kuwa waziri wa Ulinzi, wadhifa ambao alikuwa akishikilia hadi baada ya uteuzi wake kama Waziri Mkuu wa Gabon.

Rose Christiane Ossouka Raponda aliingia kwa mara ya kwaneza madarakani mnamo 2012. Ali Bongo aliteuwa kuwa Waziri wake wa Bajeti. Wadhifa uliomstahili, kwa sababu Rose Christiane Ossouka Raponda ni mchumi. Alihitimu katika Chuo Kikuu cha Uchumi na Fedha nchini Gabon.

Kazi yake kubwa kama Waziri Mkuu itakuwa ni kufufua uchumi na labda kufanya maandalizi ya uchaguzi ujao wa urais uliopangwa kufanyika mwaka 2023.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.