Pata taarifa kuu
GABON-HAKI

Alihanga, mshirika wa karibu wa Ali Bongo ahukumiwa kifungo cha miaka mitano jela

Mahakama ya nchini Gabon imemhukumu kifungo cha miaka mitano jela Brice Laccruche Alihanga, mkurugenzi mkuu wa zamani wa ofisi ya rais wa nchi hiyo Ali Bongo.

Rais wa Gabon Ali Bongo akiwa amezungukwa na Katibu Mkuu wa Ofisi ya rais Jean-Yves Teale (kushoto) na Mkurugenzi wake Brice Laccruche Alihanga mjini Libreville, Februari 2019.
Rais wa Gabon Ali Bongo akiwa amezungukwa na Katibu Mkuu wa Ofisi ya rais Jean-Yves Teale (kushoto) na Mkurugenzi wake Brice Laccruche Alihanga mjini Libreville, Februari 2019. GABONESE PRESIDENCY / AFP
Matangazo ya kibiashara

Alikuwa mwenye uwezo mkubwa wakati rais Ali Bongo alipoachia mamlaka kwa muda kutokana an maradhi ya kiharusi mwezi Oktoba 2018. Tangu wakati huo baada ya kupoteza imani kutoka kwa rais, alifungwa jela na kufunguliwa mashtaka katika kesi kadhaa. Mahakama imemhukumu kifungo cha miaka 5 jela na faini ya faranga milioni 5 za CFA.

Jaji amefuatlia kwa karibu madai ya mwendesha mashtaka wa jamhuri. Jumanne iliyopita, mwendesha mashtaka aliomba kifungo cha miaka mitano jela na faini ya faranga milioni 5 za CFA. Hatimaye Brice Laccruche Alihanga amejikuta akihukumiwa kifungo cha miaka mitano jela na kutakiwa kulipa faini hiyo ya faranga milioni 5 za CFA.

Mahakama ilikuwa ikipinga utaratibu aliotumia kupata cheti chake cha uraia wa Gabon. Mbele ya majaji siku ya Jumanne, Oktoba 26, mshirika huyo wa zamani wa Ali Bongo alishangaza kila mtu kwa kukiri ukweli ambao anatuhumiwa.

Brice Laccruche Alihanga, ambaye alizaliwa huko Marseille, nchini Ufaransa, kutoka kwa wazazi wenye uraia wa Ufaransa, alipata uraia wa Gabon akiwa na umri wa miaka 5. Baada ya kupata cheti cha uraia ambacho hakikumtaja baba yake mzazi, Fargeon, raia wa Ufaransa, lakini kilimtaja mume mwingine wa mama yake baada ya kutalakiana na babake, Alihanga, raia wa Gabon. Hata hivyo hakuna utaratibu uliopitishwa kulinagana na sheria za kuomba uraia.

Brice Laccruche Alihanga alikuwepo wakati hukumu dhii yake ilipotolewa. Mawakili wake wanasita kukata rufaa kwa wakati huu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.