Pata taarifa kuu
MSAMAHA-WAFUNGWA

Baada ya waasi, kiongozi wa utawala wa kijeshi nchini Chad awasamehe waandamanaji 259

Mkuu wa utawala wa jeshi nchini Chad, Jenerali Mahamat Idriss Déby Itno Jumatatu aliwasamehe waandamanaji 259 kati ya 262 waliohukumiwa kifungo gerezani baada ya maandamano dhidi ya utawala yaliyokandamizwa kwa umwagaji damu mnamo mwezi Oktoba 2022, siku tatu baada ya agizo kama hilo lililowaachia huru waasi 380 waliohukumiwa kifungo cha maisha.

Mahamat Idriss Déby wakati wa kuapishwa kwake kama Rais wa Mpito wa Chad.
Mahamat Idriss Déby wakati wa kuapishwa kwake kama Rais wa Mpito wa Chad. AFP - DENIS SASSOU GUEIPEUR
Matangazo ya kibiashara

Waandamanaji hawa walihukumiwa katika kesi ya halaiki iliyofunguliwa mwezi Desemba, bila wanasheria au vyombo vya habari huru, na baada ya zaidi ya mwezi mmoja na nusu kuzuiliwa katika gereza lenye ulinzi mkali katikati mwa jangwa nchini Chad, kilomita 600 kutoka mji mkuu wa Chad, N'Djamena.

Washtakiwa walikuwa wamehukumiwa kifungo cha miaka miwili hadi mitatu jela kwa "vitendo vya mkusanyiko usioidhinishwa, uharibifu wa mali, uchomaji moto wa mali, vurugu, shambulio la kukusudia, mateso na uvunjifu wa utulivu wa umma (...)" lakini sasa "wananufaika na msamaha wa rais", kulinganana agizo la rais ambalo shirika la habari la AFP limepata kopi na kutiwa saini na Jenerali Déby.

Wafungwa hawa, wengi wao wakiwa vijana, walikuwa wameitikia mwito wa kupinga kuongezwa kwa miaka miwili madarakani kwa Jenerali Déby mwezi Oktoba.

Rais huyo alitangazwa kuwa mkuu wa nchi na jeshi mnamo Aprili 20, 2021 kufuatia tangazo la kifo cha babake, Marshal wa Chad Idriss Déby Itno, aliyeuawa vitani na waasi baada ya kuongoza nchi kwa miaka 30.

"Ni ishara ya msamaha kuwaruhusu wana na mabinti wote wa Chad kujenga nchi yao katika misingi mipya," waziri wa mawasiliano na msemaji wa serikali Aziz Mahamat Saleh ameliambia shirika la habari la AFP.

Lakini uchunguzi bado haujakamilika kwa kundi jingine, ambalo "baadhi" yao wafungwa "bado wako katika gereza la Koro Toro", ameongeza Aziz Mahamat Saleh.

Uchunguzi bado unaendelea kwa watu "ishirini" waliozuiliwa N'Djamena, na wengine "mia moja " katika gereza la Koro Toro, alisema Laguerre Ndjerandi, kiongozi wa chama cha majaji huko N'Djamena.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.