Pata taarifa kuu

Chad: Rais atia saini msamaha kwa waasi 380 waliohukumiwa kifungo cha maisha jela

Nchini Chad, rais wa mpito Mahamat Idriss Déby ametia saini Jumamosi Machi 25 msamaha wa rais kwa ajili ya waasi 380 kati ya zaidi ya 400 wa kundi la waasi la Front for alternation and concord (FACT) waliohukumiwa siku ya Jumanne ya wiki iliyopita. Waasi hao walikuwa wamehukumiwa kifungo cha maisha jela kwa vitendo vya ugaidi, kuhatarisha usalama wa taifa na kuhatarisha maisha ya Mkuu wa Nchi.

Kundi la waasi wa FACT waliokamatwa, mbele ya makao makuu ya jeshi la Chad huko N'Djamena, Mei 9, 2021.
Kundi la waasi wa FACT waliokamatwa, mbele ya makao makuu ya jeshi la Chad huko N'Djamena, Mei 9, 2021. AFP - DJIMET WICHE
Matangazo ya kibiashara

Walikamatwa baada ya kifo cha aliyekuwa rais Idriss Déby mwaka wa 2021. Mwanasheria wao, Wakili Francis Lokouldé, anakaribisha uamuzi huu. "Tunaweza tu kukaribisha uamuzi huu uliochukuliwa na rais wa mpito. Tunaamini hii ni hatua kubwa, isipokuwa tunapenda kueleza kuwa huu si msamaha unaomhusu kila mtu, kwa sababu washtakiwa wapo 380 tu ambao wamesamehewa,” amesema wakili huyo.

Wakili Francis Lokoulde angependa sheria hiyo iguse kila mtu. Wafungwa hamsini na watano, akiwemo mkuu wa FACT, Mahamat Mahdi Ali, hawahusiki na msamaha huu wa rais. "Mahamat Mahdi na kundi lake hawahusiki na hatua hii. Wale wote ambao wamehukumiwa bila kuwepo hawaathiriwi na msamaha huu wa rais, anabainisha. Ni vigumu kuelewa kwa sababu pale, kama msamaha wa rais ulipaswa kuchukuliwa dhidi ya watuhumiwa wote, ingekuwa bora zaidi. Walakini, kuna kazi ya kuchagua ambayo imefanywa. "

Wakili huyo anaongeza: “Tungependa wale wote waliopatikana na hatia katika kesi hii wasamehewe. Kwa hivyo ikiwa hii ni sera ya kusaidia kutoka kwa serikali, tunataka iwe ya jumla. "

Kuachiliwa kwa wafungwa wa vita

Kwa upande wake, serikali ya Chad inaeleza kuwa dhamira ya awali ya Mkuu wa Nchi ilikuwa kuachiliwa kwa wafungwa wa vita. Na kwa hivyo kwamba watu waliohukumiwa bila kuwepo mahakamani, akiwemo Mahamat Mahdi Ali, hawawezi kunufaishwa na msamaha huu.

“Ahadi mbele ya watu wa heshima ilikuwa kuachiliwa kwa wafungwa wa vita. Watu waliohukumiwa wakiwa hawapo sio wafungwa wa vita. Mijadala hii na mazugumzo ya kurejea kwa amani daima iko wazi, na mkono unabaki kunyooshwa. Mkuu wa Nchi anaonyesha kwa kitendo hiki kwamba anajiweka juu ya vita na kwamba anataka kuchukua hatua kwa ajili ya amani na maridhiano ya uhakika ya Chad”, anaeleza Aziz Mahamat Saleh, msemaji wa serikali na Waziri wa Mawasiliano.

Baada tu ya sentensi hii, “Mahamat Idriss Déby alifikiri ulikuwa ni wakati wa kufanya kitendo hiki, ambacho zaidi ya hayo ni katika wakati muhimu kwa nchi, pamoja na kipindi cha msamaha ambacho kipindi hiki cha Ramadhani pia kinachangia. Kwa maoni yangu, ni kitendo cha nguvu, kitendo ambacho kina ishara muhimu kwa taifa la Chad, kuruhusu kweli kuweza kujenga upya misingi mipya, "anahakikishia msemaji wa serikali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.