Pata taarifa kuu
SIASA-HAKI

Maandamano nchini Chad: Washtakiwa 262 wahukumiwa kifungo cha miaka miwili na mitatu jela

Jumla ya watu 262 waliokamatwa huko N'Djamena wakati wa maandamano yaliyokandamizwa kwa nguvu mwezi Oktoba, huku takriban watu 50 wakiwa wamepigwa risasi na kuuawa, wamehukumiwa kifungo cha miaka 2 hadi 3 jela katika kesi ya watu wengi bila ya mawakili, mwendesha mashtaka ametangaza siku ya Jumatatu.

Watu waliuawa na wengine kujeruhiwa wakati wa maandamano dhidi ya kuendelea kwa madaraka ya Mahamat Déby, Oktoba 2022.
Watu waliuawa na wengine kujeruhiwa wakati wa maandamano dhidi ya kuendelea kwa madaraka ya Mahamat Déby, Oktoba 2022. © HYACINTHE NDOLENODJI via REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Baadhi ya watu 80, kati ya watu 401 waliohukumiwa, hasa waandamanaji dhidi ya serikali, wamehukumiwa kifungo jela na 59 waliachiliwa huru, mwendesha mashtaka wa N'Djamena, Moussa Wade, amewaambia waandishi wa habari.

Kesi hii ya watu wengi imefanyika katikati ya jangwa, kilomita 600 kutoka mji mkuu, katika gereza lenye ulinzi mkali huko Koro Toro, utaratibu "haramu" wa kuwahamisha watu kutoka nje kwa mujibu wa wanasheria wao ambao waliamua kutohudhuria kesi hiyo. Wamehukumiwa hasa kwa "vurugu na shambulio", "uharibifu wa mali" na "kuyumbisha usalama".

Kesi hiyo imefanyika kwa muda wa siku nne na kumalizika siku ya Ijumaa, lakini televisheni ya taifa pekee ndiyo iliyokuwa na haki ya kuhudhuria, bila ya kuwepo vyombo vingine vya habari, mwendesha mashtaka hakutoa hukumu hiyo hadharani lakini siku tatu baadaye, aliporejea mji mkuu.

Success Masra, rkongozi wa chama cha Les Transformateurs, aliambia shirika la habari la AFP siku ya Jumatano kwamba alilazimika kujificha kwa sababu za kiusalama.

Mnamo Oktoba 20, 2022, karibu watu hamsini, idadi kubwa ya waandamanaji vijana waliouawa kwa risasi, walikufa huko N'Djamena na kwingineko wakati polisi walipofyatua risasi kwenye wakati walipokuwa wakijaribu kukusanyika.

Walikuwa wakiitikia mwito wa upinzani dhidi ya kuongezwa kwa miaka miwili madarakani kwa Jenerali Mahamat Idriss Déby Itno, aliyetangazwa kuwa mkuu wa nchi na jeshi mnamo Aprili 20, 2021 kufuatia tangazo la kifo cha baba yake, Rais Idriss Déby Itno, aliyeuawa vitani na waasi baada ya kuitawala Chad kwa mkono wa chuma kwa miaka 30.

Baadhi ya watoto 80 waliozuiliwa Koro Toro wamehamishiwa N'Djamena, mwendesha mashtaka Wade Djibrine almesema Jumatatu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.