Pata taarifa kuu
USHIRIKIANO-DIPLOMASIA

Kabla ya ziara yake Afrika ya Kati, Emmanuel Macron atathimini sera yake ya Afrika

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron atatoa, Jumatatu, Februari 27, hotuba mpya juu ya mwelekeo wa sera yake ya Afrika katika miaka ijayo. Hotuba hii inakuja kabla ya kuanza kwa safari yake katika nchi nne za Afrika ya Kati: Gabon, Angola, Kongo na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron anaongea kutoka ikulu ya Elysée huko Paris mnamo Januari 22, 2023.
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron anaongea kutoka ikulu ya Elysée huko Paris mnamo Januari 22, 2023. AP - Benoit Tessier
Matangazo ya kibiashara

Katika hotuba Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ataonyesha "vipaumbele vyake na njia yake ya kukuza ushirikiano kati ya Ufaransa, Ulaya na bara la Afrika", inaelezea ikulu ya Élysée. Pia ataonyesha jinsi Paris inavyozingatia mabadiliko ya uwepo wake wa kijeshi kwenye bara hilo, wakati jeshi la Ufaransa lililazimika kuondoka Mali na Burkina Faso, ambapo lilihusika katika hatua za pamoja za kupambana dhidi ya ugaidi.

"Falsafa ya mabadiliko haya ni kushirikiana katika njia nyingine, sio tena kutuma vikosi Afrika," mshauriwa rais ameliambia shirika la habar la AFP. "Tunaingia kwenye mzunguko ambao tutafanya kazi katika mtazamo mwingine," ameongeza.

► Soma pia: Rais wa Ufaransa kuzuru nchi nne za Afrika ya Kati kwa lengo la kuimarisha ushirikiano

Hotuba hii ya rais wa Ufaransa inakuja baada ya ile ya Ouagadougou mnamo Novemba 2017, ambayo Emmanuel Macron aliendeleza kanuni alizokusudia kuweka wakati wa kipindi chake cha kwanza cha miaka mitano katika sera ya Afrika ya Ufaransa.

Hatua hii ya Rais Macron inataka kuimariha sera yake katika muhula wake wa pili. Inafika katika muktadha ambapo, katika bara hilo, uhusiano wa Ufaransa na koloni zake za zamani husababisha mijadala zaidi na mikubwa kwa vijana wanaotamani kubuni aina mpya ya uhusiano wa kimataifa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.