Pata taarifa kuu
USHIRIKIANO-DIPLOMASIA

Macron kutangaza mkakati wake kwa Afrika siku ya Jumatatu

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron atawasilisha mkakati wake kwa Afrika kwa miaka minne ijayo siku ya Jumatatu ili "kuimarisha ushirikiano kati ya Ufaransa, Ulaya na bara la Afrika," ikulu ya Elysée imetangaza siku ya Ijumaa.

Emmanuel Macron atazuru nchi nne za Afrika ya Kati wiki ijayo: Gabon, Angola, Kongo na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Emmanuel Macron atazuru nchi nne za Afrika ya Kati wiki ijayo: Gabon, Angola, Kongo na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. AP - Geert Vanden Wijngaert
Matangazo ya kibiashara

Katika hotuba yake katika ikulu ya Elysée, siku mbili kabla ya kuanza kwa ziara yake Afrika ya Kati, amebainisha "maono yake ya ushirikiano na nchi za Afrika" na "njia anayoweka" kwa muhula wake wa pili wa miaka mitano, amesema mshauri wa rais.

Emmanuel Macron atazuru nchi nne za Afrika ya Kati wiki ijayo: Gabon, Angola, Kongo na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. "Ataweka malengo ya safari hii na, kwa upana zaidi, vipaumbele vyake na mbinu yake ya kuimarisha ushirikiano kati ya Ufaransa, Ulaya na bara la Afrika," imesema Elysée katika taarifa yake kwa vyombo vya habari.

Hotuba hii, iliyopangwa saa kumi na moja jioni, imefuatiwa na mkutano na waandishi wa habari wa Ufaransa na Afrikakwa njia ya video.

Rais wa Jamhuri ataweza "kueleza zaidi mabadiliko ya uwepo wetu wa kijeshi barani Afrika, mageuzi ambayo kimsingi yanahusu Afrika Magharibi lakini pia Afrika ya Kati", amebainisha mshauri.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.