Pata taarifa kuu
USHIRIKIANO-DIPLOMASIA

Rais wa Ufaransa kuzuru nchi nne za Afrika ya Kati kwa lengo la kuimarisha ushirikiano

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, kuanzia wiki ijayo, atazuru mataifa manne ya Afrika ya Kati, ziara inayolenga kupunguza ushawishi wa China na Urusi katika ukanda huo.

Ziara ya Emmanuel Macron inakuja katika kipindi ambacho, Urusi inaaminiwa kuendeleza ushirikiano wa karibu na mataifa yanayozungumza lugha ya Kifaransa, lakini pia China ikiongeza kiwango chake cha uwekezaji kwa nchi hizo.
Ziara ya Emmanuel Macron inakuja katika kipindi ambacho, Urusi inaaminiwa kuendeleza ushirikiano wa karibu na mataifa yanayozungumza lugha ya Kifaransa, lakini pia China ikiongeza kiwango chake cha uwekezaji kwa nchi hizo. AP - Geert Vanden Wijngaert
Matangazo ya kibiashara

Macron ataanzia ziara yake nchini Gabon tarehe 1 mwezi Machi, atakapohudhuria mkutano wa mazingira, kabla ya kwenda Angola, Congo-Brazavile na hatimaye Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. 

Ziara yake inakuja katika kipindi ambacho, Urusi inaaminiwa kuendeleza ushirikiano wa karibu na mataifa yanayozungumza lugha ya Kifaransa, lakini pia China ikiongeza kiwango chake cha uwekezaji kwa nchi hizo. 

Paris inaishtumu Moscow kwa kulenga kusambaza taarifa potovu kwa lengo la kuathiri maslahi yake katika koloni zake za zamani. 

Macron ambaye alichaguliwa tena kuongoza Ufaransa mwaka uliopita, alisema bara la Afrika ni jukumu la pili katika uongozi wake na mwezi Julai, alizuru Cameroon, Benin na Guinea Bissau. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.