Pata taarifa kuu
USALAMA-ULINZI

Ofisi ya tume ya uchaguzi na kituo cha polisi vyashambuliwa nchini Nigeria

Watu waliokuwa na silaha nzito walishambulia ofisi ya Tume ya Uchaguzi na kituo cha polisi kusini mashariki mwa Nigeria siku ya Jumatano, na kumuua kijana mmoja na kumjeruhi mwingine, wiki tatu kabla ya uchaguzi wa urais, kulingana na vyanzo vya serikali.

Mnamo Februari 25, Wanigeria watamchagua mrithi wa Rais Muhammadu Buhari, jenerali wa zamani ambaye hawania tena katika uchaguzi wa urais baada ya mihula miwili ambayo haijawezesha kuzuia matatizo makubwa ya usalama ambayo yanaikumba nchi hiyo.
Mnamo Februari 25, Wanigeria watamchagua mrithi wa Rais Muhammadu Buhari, jenerali wa zamani ambaye hawania tena katika uchaguzi wa urais baada ya mihula miwili ambayo haijawezesha kuzuia matatizo makubwa ya usalama ambayo yanaikumba nchi hiyo. AFP - KOLA SULAIMON
Matangazo ya kibiashara

Mnamo Februari 25, Wanigeria watamchagua mrithi wa Rais Muhammadu Buhari, jenerali wa zamani ambaye hawania tena katika uchaguzi wa urais baada ya mihula miwili ambayo haijawezesha kuzuia matatizo makubwa ya usalama ambayo yanaikumba nchi hiyo: uasi mkali wa wanajihadi kaskazini mashariki, mvutano wa kujitenga kusini mwa nchi, kuongezeka kwa uhalifu kaskazini-magharibi na katikati.

Siku ya Jumatano asubuhi, watu waliokuwa wakiwasili wakiwa na magari manne na hasa wakiwa na "vilipuzi vilivyoboreshwa" walishambulia ofisi ya Tume ya Uchaguzi (INIC), kituo cha polisi na jengo la makazi linalopakana na kituo cha polisi, kulingana na taarifa kwa vyombo vya habari kutoka polisi ya Jimbo la Anambra (kusini mashariki). "Kwa bahati mbaya, mvulana mwenye umri wa miaka 16, ndugu wa afisa mmoja wa polisi, aliuawa na watu wenye silaha, huku msichana wa miaka 15 akipata majeraha ya risasi," imesema taarifa hiyo.

Msichana huyo alipelekwa hospitalini ambako amelazwa kwa sasa. Jengo la Tume ya uchaguzi "liliharibiwa vibaya", kulingana na taarifa kwa vyombo vya habari iliyotiwa saini na mwenyekiti wa INEC, Festus Okoye.

IEC hivi majuzi ilionya kuhusu tishio la kuongezeka kwa ghasia wakati wa kampeni za uchaguzi, na kuongeza kuwa imerekodi angalau mashambulizi 50 tangu kuzinduliwa kwake karibu miezi miwili iliyopita. Ingawa hakuna kundi lililodai kuhusika na shambulio hilo jipya, kusini-mashariki mwa Nigeria limekuwa eneo la mashambulizi mengi yanayohusishwa kundi la wanaharakati wanaotetea Uhuru wa wakaazi wa Biafra (IPOB).

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.