Pata taarifa kuu
UCHAGUZI-SIASA

Uchaguzi wa urais wa Nigeria: Wagombea wakuu watukanana hadharani

Wagombea nchini Nigeria wamemaliza kampeni, kila mmoja akitoa wito wa kukamatwa kwa mwingine wakishtumiana kashfa za zamani za ufisadi. "Ugonjwa wa Parkinson", "bahili", "ufisadi": hayo ni maneo ambayo wagombea wawili wakuu katika uchaguzi wa urais nchini Nigeria wamekuwa wakitoleana.

Zaidi ya Wanigeria milioni 93 wataitwa kupiga kura kumchagua mrithi wa Rais Muhammadu Buhari, ambaye hatagombea mihula miwili.
Zaidi ya Wanigeria milioni 93 wataitwa kupiga kura kumchagua mrithi wa Rais Muhammadu Buhari, ambaye hatagombea mihula miwili. AFP - KOLA SULAIMON
Matangazo ya kibiashara

Siasa za Nigeria zinakabiliwa na shutuma za kila aina, hasa kuhusu masuala ya pesa zinazopatikana kwa njia haramu. Na waliopendekezwa katika uchaguzi wa urais mnamo Februari 25 - ni Bola Tinubu na Atiku Abubakar, wote matajiri: wameshutumiwa mara kwa mara kwa rushwa, ambayo wanakanusha vikali.

Zaidi ya Wanigeria milioni 93 wataitwa kupiga kura kumchagua mrithi wa Rais Muhammadu Buhari, ambaye hatagombea mihula miwili. Taifa lenye watu wengi zaidi barani Afrika linakabiliwa na changamoto nyingi, hususan ukosefu wa usalama unaokaribia kuenea nchi nzima, mzozo mkubwa wa kiuchumi na ukosefu wa usawa unaoendelea. Katika wiki za hivi karibuni, wakati kampeni zikishika kasi, matusi na shutuma zimepamba moto baina ya wagombea.

Bola Ahmed Tinubu, mgombea wa chama tawala (APC), hivyo anamshutumu Atiku Abubakar, wa upinzani (PDP), kwa "kuendesha biashara ya uhalifu na kujenga himaya kwa njia ya udanganyifu" kwa "kuiba fedha za umma" kati ya mwaka 1999 na 2007, wakati alipokuwa makamu wa rais.

Bw. Tinubu, aliyepewa jina la utani la "Godfather" au hata "The Boss" kwa ushawishi na utajiri wake mkubwa, anatoa wito kwa mpinzani wake "kujiondoa katika kinyang'anyiro cha urais mara moja" na "kujisalimisha kwa vyombo vya sheria". Anamwita Bwana Abubakar "Bwana nauza kila kitu", akimtaja kuwa "tayari kupata risiti" na kumwita "mfisadi".

Uchunguzi wa Bunge la Seneti la Marekani unataja jina la Bw. Abubakar katika kesi ya utakatishaji fedha. Kati ya mwaka wa 2000 na 2008, mmoja wa wake zake wakati huo, ambaye ana uraia wa Marekani, anadaiwa "kumsaidia mumewe kurejesha zaidi ya dola milioni 40 za fedha zinazotiliwa shaka na Marekani kupitia akaunti za nje ya nchi", kulingana na ripoti hiyo.

Wanandoa hao pia wanatuhumiwa kupokea zaidi ya dola milioni 2 kwa kandarasi na kampuni ya kimataifa ya Siemens, ambayo ilikiri hatia katika kesi hii.

Majibu ya kukasirisha kutoka kwa kambi ya Atiku Abubakar kukataa 'uongo' wa APC: Bwana Abubakar ana 'tabia isiyo na kifani na uadilifu'... Tofauti na mpinzani wake 'aliyeharibiwa na mihadarati' , sentensi iliyojaa innuendo.

Bw. Tinubu anatuhumiwa kuwa, katika ujana wake, alipokuwa mhasibu nchini Marekani, aliiba pesa kwa niaba ya mtandao mkubwa wa ulanguzi wa heroini, jambo ambalo anakanusha. Akiwa na umri wa miaka 70, mgombea wa APC, gavana wa zamani wa Lagos, mara kwa mara amekuwa akishutumiwa kwa rushwa, bila kuhukumiwa.

Timu ya "Atiku" pia inataka kukamatwa kwa Bw. Tinubu, anayetuhumiwa kuandaa "jeshi la majambazi" "kudhoofisha" uchaguzi wa Februari 25. Kabla ya kuendelea: "Mgombea wa APC lazima awe na ugonjwa wa Parkinson unaoambatana na kutoweza kujizuia". Bola Tinubu "hawezi kusimama moja kwa moja au kupanda (ngazi) bila msaada, anaugua tetemeko linaloonekana mikononi mwake", wanasema.

Afya ya wagombea urais ni suala nyeti nchini Nigeria, ambapo Rais Buhari alizua gumzo kubwa kwa kutohudhuria kwa miezi kadhaa wakati wa muhula wake wa kwanza kutafuta matibabu nchini Uingereza kwa ugonjwa usiojulikana.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.