Pata taarifa kuu
CHINA- AFYA

China yakashifu vikwazo vya usafiri kwa raia wake

Serikali ya China imesema kitendo cha mataifa mbalimbali duniani kuweka vikwazo kwa wasafiri wanaotoka nchini mwake kutokana na UVIKO19 “Haikubaliki” wakati huu nchi zaidi zikisema zitaendelea kuwapima virusi hivyo raia kutoka Beijing.

Hali ya Uviko 19 nchini China
Hali ya Uviko 19 nchini China VIA REUTERS - CHINA DAILY
Matangazo ya kibiashara

Marekani, Canada, Ufaransa na Japan, ni miongoni mwa nchi ambazo zinahitaji wasafiri kutoka China kuonyesha vipimo vya kutokuwa na Uviko 19, wakati huu nchi hiyo ikirekodi ongezeko la maambukizi.

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa China Mao Ning, amesema hatua hiyo inakosa misingi ya kisayansi kwa kuzuia raia kutoka China pekee, wakati baadhi ya nchi zikitaja ukosefu wa uwazi wa China kuhusu takwimu za maambukizo.

Katika siku za hivi karibuni, China imeshuhudia ongezeko la maambukizo, ambapo mwishoni mwa mwezi Disemba mwaka uliopita, Beijing ilisema wasafiri wanaoingia nchini humo hawatahitajika kuwekwa karantini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.