Pata taarifa kuu

Nigeria: Raia kadhaa wakamatwa kwa kupanga 'harusi ya wapenzi wa jinsia moja '

Polisi ya Kiislamu wamewakamata watu 19 wanaotuhumiwa kupanga harusi ya wapenzi wa jinsia moja katika mji wa Kano ulioko kaskazini mwa Nigeria, msemaji wa polisi amesema siku ya Jumanne.

Jiji la Kano, Nigeria. Hii si mara ya kwanza kwa polisi ya Kiislamu kuwakamata, wakiwatuhumu vijana kuandaa ndoa za wapenzi wa jinsi moja.
Jiji la Kano, Nigeria. Hii si mara ya kwanza kwa polisi ya Kiislamu kuwakamata, wakiwatuhumu vijana kuandaa ndoa za wapenzi wa jinsi moja. AFP - PIUS UTOMI EKPEI
Matangazo ya kibiashara

Kano ni mojawapo ya majimbo 12 kaskazini mwa Nigeria yaliyoanzisha Sharia mwaka 2000, ambapo mahakama za Kiislamu zinafanya kazi pamoja na mfumo wa sheria wa serikali.

Hii si mara ya kwanza kwa polisi ya Kiislamu kuwakamata, wakiwatuhumu vijana kuandaa ndoa za wapenzi wa jinsi moja. Kila mara washukiwa hao walikanusha wakisema walikuwa wamekusanyika kwa tafrija. Ushoga unaadhibiwa na kifo chini ya sheria ya Kiislamu, lakini hakuna hukumu ya kifo iliyowahi kutolewa hadi sasa.

Watu hao 19, wanawake 15 na wanaume wanne walio na umri wa miaka zaidi ya ishirini, walikamatwa siku ya Jumapili katika chumba cha kazi nyingi, Lawan Ibrahim Fagge, msemaji wa polisi wa Kiislamu, ameliambia shirika la habari la AFP. "maafisa wetu wa polisi walivamia ukumbi ambapo wanandoa wa jinsia moja walikuwa wakipanga harusi na kuwakamata wanaume na wanawake 19, akiwemo muandaaji harusi," ameongeza.

Fagge, hata hivyo, alisema wanandoa wawili wanaoshukiwa walifanikiwa kutoroka na polisi inawasaka. Kulingana na msemaji huyo, washukiwa hao wamezuiliwa wakati huo huo wakisubiri uchunguzi kamili.

Mnamo mwaka wa 2014, nchi yenye watu wengi zaidi barani Afrika - ya kidini sana - ilipitisha sheria dhidi ya ndoa za jinsia moja. Tangu wakati huo, ushoga unaadhibiwa kwa miaka 10 hadi 14 jela. Polisi ya Kiislamu, "Hisbah" huko Kano, katika siku za nyuma iliwakamata watu kadhaa wanaotuhumiwa kupanga ndoa za wapenzi wa jinsi moja, bila hata hivyo kuhukumiwa.

Mnamo 2018, Hisbah ilikamata wasichana 11 walioshtakiwa kupanga ndoa ya wapenzi wa jinsi moja. Walikanusha shtaka hilo, wakisema kwamba wao ni wa klabu ya densi na walitaka kusherehekea uteuzi wa mkuu wa klabu yao.

Mnamo mwezi Januari 2015, Hisbah ilikamata vijana 12 katika hoteli katika viunga vya Kano, wanaoshukiwa kupanga ndoa ya wapenzi wa jinsia moja. Vijana hao pia walikanusha, wakisema walikuwa wakiandaa sherehe ya maadhimishp ya kuzaliwa kwa rafiki yao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.