Pata taarifa kuu

Nigeria: Zaidi ya wanakijiji 20 wauawa na watu wenye silaha katika Jimbo la Kaduna

Zaidi ya wanakijiji 20 wameuawa katika mashambulizi mawili tofauti ya watu wenye silaha katika jimbo lenye machafuko la Kaduna, kaskazini mwa Nigeria, ambayo inaongoza kwa idadi ya watu wengi barani Afrika, maafisa wa eneo hilo wamesema. Kaduna ni mojawapo ya majimbo yaliyoathiriwa zaidi na "majambazi".

Gari la kijeshi likishika doria katika mitaa ya Kaduna, Nigeria.
Gari la kijeshi likishika doria katika mitaa ya Kaduna, Nigeria. AFP - KOLA SULAIMON
Matangazo ya kibiashara

Idadi ya vifo vya vurugu za Jumapili dhidi ya vijiji vya Malagum 1 na Sakwong, katika wilaya ya Kaura, ni 28 au 37 kulingana na vyanzo.

Magenge ya wahalifu kwa miaka kadhaa yamekuwa yakishambulia vijiji vya kaskazini-magharibi na katikati mwa nchi ili kuiba ng'ombe, kuwateka nyara wakaazi ili kuwakomboa kwa kutoa fidia, kupora chakula na kuchoma nyumba.

Atuk Stephen, mmoja wa maafisa wa wilaya ya Kaura, ameiambia televisheni ya ndani kuwa watu 37 wameuawa na majambazi, ambao wamechoma moto zaidi ya nyumba 100 na magari kadhaa.

Vyanzo vingine vya habari viliripoti kuwa watu 28 wameuawa.

Kamishna wa Masuala ya Ndani ya Jimbo la Kaduna, Samuel Aruwan, amethibitisha kuwa mashambulizi hayo yamesababisha vifo vya watu kadhaa, lakini haikutoa idadi kamili na ya uhakika. Ameongeza kuwa jeshi limejipanga katika eneo hilo kuwasaka washambuliaji.

Hali hii inachangiwa na wakati mwingine mapigano makali kati ya wafugaji wa ng'ombe wanaohamahama na wakulima wa eneo hilo kuhusu haki za malisho na maji, mapigano ambayo yamechukua mwelekeo wa kikabila na kidini.

Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari yuko chini ya shinikizo kubwa la kukomesha ghasia kabla ya kuondoka madarakani mwaka ujao baada ya kumaliza muhula wa miaka minane.

"Majambazi", wanaotajwa kama "magaidi" na serikali ya shirikisho, wanachochewa na maslahi. Lakini wachambuzi wana wasiwasi kuhusu kukua kwa uhusiano na makundi ya kijihadi kaskazini mashariki, ambayo yamekuwa yakiongoza uasi kwa miaka 13.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.