Pata taarifa kuu

Nigeria: Maafisa wanne wa Polisi na raia 2 wauawa na watu wenye silaha

Watu wenye silaha walishambulia doria ya polisi siku ya Jumatatu karibu na soko moja kaskazini-magharibi mwa Nigeria, karibu na mpaka na Niger, na kuwaua maafisa wanne wa polisi na raia wawili, polisi imesema.

Rais Muhammadu Buhari anakosolewa vikali na wakosoaji baada ya mihula miwili iliyokubwa na kuongezeka kwa ukosefu wa usalama, miezi miwili na nusu kabla ya uchaguzi wa rais ambao hatawaia tena, kwa mujibu wa Katiba.
Rais Muhammadu Buhari anakosolewa vikali na wakosoaji baada ya mihula miwili iliyokubwa na kuongezeka kwa ukosefu wa usalama, miezi miwili na nusu kabla ya uchaguzi wa rais ambao hatawaia tena, kwa mujibu wa Katiba. AFP - KOLA SULAIMON
Matangazo ya kibiashara

 

Kaskazini na katikati mwa Nigeria ni eneo linalokabiliwa na makundi ya wahalifu, wanaoitwa  nchini humo"majambazi", ambao hushambulia na kupora vijiji, kuua wakaazi wa vijiji hivyo au kuwateka nyara kwa kutarajia kulipwa fidia.

Washambuliaji waliofika kwa pikipiki walifyatulia risasi gari la polisi lililokuwa limeegeshwa nje ya soko katika kijiji cha Yar Bulutu, wilaya ya Sabon Birni, jimbo la Sokoto.

"Tulipoteza maafisa wanne wa polisi katika shambulio la majambazi, pia waliwapiga risasi raia wawili," Sanusi Abubakar, msemaji wa polisi wa jimbo la Sokoto, ameliambia shirika la habari la AFP. Baada ya tukio tulizindua operesheni ya kuwasaka na tuna uhakika watakamatwa," ameongeza.

Kulingana na chanzo hiki, shambulio hili lilifanywa kwa kulipiza kisasi kwa hasara iliyowakuta "majambazi" hao wiki iliyopita. Majambazi kadhaa waliuawa na polisi walipozima shambulio kwenye kijiji katika wilaya jirani ya Silman.

Ukosefu wa usalama nchini Nigeria, nchi yenye watu wengi zaidi barani Afrika, umeenea kote nchini. Kila siku, nchi inakumbwa na ghasia zinazofanywa na makundi ya wahalifu au wanajihadi, na mamlaka zinazoshutumiwa kuwa miongoni mwa mafisadi zaidi duniani, haziwezi kukomesha hali hiyo.

Rais Muhammadu Buhari anakosolewa vikali na wakosoaji baada ya mihula miwili iliyokubwa na kuongezeka kwa ukosefu wa usalama, miezi miwili na nusu kabla ya uchaguzi wa rais ambao hatawaia tena, kwa mujibu wa Katiba.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.