Pata taarifa kuu

Zambia: Polisi yafungua uchunguzi baada ya kupatikana kwa wahamiaji 27 Lusaka

Wahamiaji 26 wa Ethiopia walipatikana wamekufa Jumapili, Desemba 11 kwenye ukingo wa barabara kaskazini mwa Lusaka, mji mkuu wa Zambia. Nchi ambayo hutumika kama kivuko cha uhamiaji haramu kwenda Afrika Kusini. Polisi imefungua uchunguzi.

Lusaka, mji mkuu wa Zambia.
Lusaka, mji mkuu wa Zambia. © Getty Images/Stuart Fox
Matangazo ya kibiashara

Wakazi wa wilaya ya Ngwerere, vitongoji vya Lusaka, ndio walotoa taarifa kwa polisi baada ya kugundua miili hiyo kando ya barabara alfajiri ya Desemba 11.

Mara baada ya hapo, polisi walimkuta mtu bado yu hai na "akihema" kati ya miili iliyotupwa kando ya barabara. Alikimbizwa hospitalini. Wengine 26 walipelekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti kwa uchunguzi wa maiti. Polisi imefungua uchunguzi, lakini tayari imebainisha katika taarifa kwa vyombo vya habari kwamba watu hao ni wanaume wenye umri wa miaka 20 hadi 38, pengine ni raia wa Ethiopia waliokufa kwa "njaa na uchovu".

Zambia ni mojawapo ya nchi zinazopitisha wahamiaji kutoka Afrika Mashariki wanaojaribu kufika Afrika Kusini kinyume cha sheria kutafuta ajira. Mnamo mwezi Oktoba, miili 30 ya wahamiaji wa Ethiopia waliopoteza maisha ilipatikana nchini Malawi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.