Pata taarifa kuu
MAREKANI- AFRIKA

Mkutano kati ya Marekani na viongozi wa Afrika waanza Jijini Washington

Mkutano wa siku tatu kati ya viongozi wa mataifa ya Afrika na Marekani, umeanza jijini Washington.

Rais wa Marekani Joe Biden
Rais wa Marekani Joe Biden AP - Andrew Harnik
Matangazo ya kibiashara

Katika mkutano huo, rais Joe Biden anatarajiwa kuwahakikishia viongozi hao wa Afrika, ushirikiano wa serikali yake, wakati huu Marekani ikisema, itatoa msaada wa fedha wa Bilioni 55 kwa mataifa ya Afrika kwa ajili ya maendeleo kwa kipindi cha miaka mitatu ijayo.

Jake Sullivan ni mshauri wa masuala ya usalama katika Ikulu ya Marekani anaeleza lengo la mkutano huo.

Hii itahusu kile tunachoweza kutoa, Itakuwa pendekezo chanya kuhusu Marekani na ushirikiano na Afrika, Haitahusu nchi zingine, Haitakuwa kujaribu kulinganisha mataifa.” Amesema Sullivan.

Hali ya usalama Mashariki mwa DRC na hali ya Jimbo la Tigray inajadiliwa pembezoni mwa mkutano huu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.