Pata taarifa kuu

Makubaliano ya amani huko Tigray: Abiy Ahmed anasema amepata "100%" ya madai yake

Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed amesema Alhamisi wiki hii kwamba amepata "asilimia 100" ya kile ambacho serikali yake ilikuwa inaomba, katika makubaliano yaliyotiwa saini Jumatano na mamlaka ya waasi ya eneo la Tigray kumaliza mzozo wa miaka miwili kaskazini mwa Ethiopia.

"Katika mazungumzo ya Afrika Kusini, asilimia 100 ya hoja zilizopendekezwa na Ethiopia yamekubaliwa," Abiy Ahmed amejigamba Alhamisi wiki hii mbele ya umati wa wafuasi wake huko Arba Minch, kusini mwa nchi.
"Katika mazungumzo ya Afrika Kusini, asilimia 100 ya hoja zilizopendekezwa na Ethiopia yamekubaliwa," Abiy Ahmed amejigamba Alhamisi wiki hii mbele ya umati wa wafuasi wake huko Arba Minch, kusini mwa nchi. AP
Matangazo ya kibiashara

Makubaliano hayo, yaliyohitimishwa mjini Pretoria ambako pande hizo mbili zimekuwa zikijadiliana tangu Oktoba 25 chini ya mwavuli wa Umoja wa Afrika, yaeleza kusitishwa mara moja kwa mapigano, kupokonywa silaha kwa vikosi vya waasi na kuwasilisha misaada ya kibinadamu.

"Katika mazungumzo ya Afrika Kusini, asilimia 100 ya hoja zilizopendekezwa na Ethiopia yamekubaliwa," Abiy Ahmed amejigamba Alhamisi wiki hii mbele ya umati wa wafuasi wake huko Arba Minch, kusini mwa nchi.

"Miongoni mwa ushindi uliopatikana (katika makubaliano), uhuru na uadilifu wa eneo la Ethiopia umekubaliwa na pande zote mbili", amesisitiza, pamoja na kanuni ya "kikosi kimoja chenye silaha katika nchi husika".

Mkataba huo haujachapishwa, lakini tamko la pamoja lililosomwa hadharani na wajumbe linaonyesha muhtasari wake mpana. Makubaliano hayo yanahusu upokonyaji silaha kwa vikosi vya mamlaka ya waasi huko Tigray.

Lakini hauelezi utaratibu na hauangazii mustakabali wa vikosi ambavyo majimbo ya kikanda ya nchi hiyo yana vifaa, au uwepo katika ardhi ya Ethiopia ya jeshi la nchi jirani ya Eritrea, ambalo limetoa msaada muhimu kwa jeshi la Ethiopia huko Tigray. .

Vyombo vya habari haviwezi kufika kaskazini mwa Ethiopia na mawasiliano huko yanafanya kazi bila mpangilio, na hivyo kufanya kuwa vigumu kujua kama usitishaji mapigano unaheshimiwa.

Ripoti ya mzozo huo, uliogubikwa na dhuluma zisizohesabika na zinazofanyika kwa siri, haijulikani, lakini shirika la kimataifa linalotatua migogoro, International Crisi Group, (ICG) na Amnesty International (AI) zinauelezea kama "mojawapo ya mgogoro mbaya zaidi duniani".

Mzozo huo ulianza Novemba 4, 2020, wakati Abiy Ahmed alipotuma jeshi la shirikisho kuwakamata viongozi wa afisa mkuu wa Tigray ambaye alikuwa amepinga mamlaka yake kwa miezi kadhaa na ambaye aliwashutumu kwa kushambulia kambi ya kijeshi la shirikisho.

Vita hivyo vimesababisha maafa ya kibinadamu kaskazini mwa Ethiopia, na kuwafanya zaidi ya Waethiopia milioni mbili kuyahama makazi yao na kuwatumbukiza mamia kwa maelfu katika hali ya njaa, kulingana na Umoja wa Mataifa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.