Pata taarifa kuu

Sam Matekane, mshindi wa uchaguzi atawazwa Lesotho

Waziri Mkuu mpya wa Lesotho, tajiri mkuu wa almasi katika siasa Sam Matekane, ambaye alizua mshangao katika uchaguzi wa wabunge mwanzoni mwa mwezi wa Oktoba, ametawazwa leo Ijumaa katika uwanja wa michezo huko Maseru, mji mkuu wa nchi ndogo ya kifalme, kusini mwa Afrika.

"Ninapendekeza mkataba wa kijamii ili kuifanya Lesotho kuwa kubwa tena," Waziri Mkuu mpya wa Lesotho Sam Matekane amesema.
"Ninapendekeza mkataba wa kijamii ili kuifanya Lesotho kuwa kubwa tena," Waziri Mkuu mpya wa Lesotho Sam Matekane amesema. © Molise Molise / AFP
Matangazo ya kibiashara

Mfanyabiashara huyo mwenye umri wa miaka 64, ambaye alifika katika gari aina ya Rolls Royce akisindikizwa na farasi na pikipiki, amesema anataka kupunguza matumizi ya serikali. Ameahidi kuchapisha ukaguzi wa mtindo wake wa maisha ndani ya mwezi mmoja, kama sehemu ya mpango wake wa "kusahihisha makosa ya kihistoria ya nchi yetu".

"Ninapendekeza mkataba wa kijamii ili kuifanya Lesotho kuwa kubwa tena," ameuambia umati wa watu uliokuwa na furaha, ambapo ameahidi "kufikia utulivu wa kiuchumi" na "kukomesha ufujaji wa fedha za umma uliokithiri".

Bw Matekane aliteuliwa kuwa waziri mkuu na mfalme na kuunda serikali ya mseto, baada ya chama chake cha Revolution for Prosperity (RFP), kilichoundwa miezi sita kabla ya uchaguzi wa Oktoba 7, kushinda viti 56 kati ya 120 bungeni.

Viongozi kadhaa wa nchi kutoka kanda hiyo, akiwemo Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa, walikuwepo kwenye hafla hiyo, pamoja na maelfu ya raia wa kawaida, waliovalia mavazi ya rangi ya chama cha RFP na vyama vidogo vilivyojiunga na muungano wa Bw. Matekane.

"Uhusiano mkubwa wa mataifa yetu mawili unategemea uhusiano wa kifamilia, lugha ya pamoja, historia... maisha yetu ya zamani hayatenganishwi na maisha yetu ya baadaye yameunganishwa," amesema Bw Ramaphosa, ambaye nchi yake inazunguka kabisa nchi hii ndogo ya kifalme tangu 1966.

Katika mahojiano na shirika la habari la AFP kabla ya kuchaguliwa kwake, Bw. Matekane, kutoka familia ya watu maskini, alisema anataka kufufua uchumi na miundombinu ya nchi, ambayo ni miongoni mwa nchi maskini zaidi duniani, na kuondokana na madeni ya umma. "Nchi yetu inatumbukia: sisi wafanyabiashara lazima tuiokoe," alisema, akishawishika kuwa kuendesha serikali hakuna tofauti na kuendesha biashara.

Lesotho imekumbwa na msukosuko wa muda mrefu wa kisiasa unaotokana na mfululizo wa mapinduzi na watu watu kulazimika kuyahama makazi yao, na ambapo Mfalme Letsie III hana mamlaka.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.