Pata taarifa kuu
LESOTHO- SIASA.

Lesotho: Waziri mkuu wa zamani ameondolewa mashtaka ya mauwaji

Lesotho imeuondelea mashtaka ya mauwaji aliyekuwa waziri mkuu wa zamani nchini humo Thomas Thabane na mkewe baada yao kutuhumiwa kuhusika na mauwaji ya aliyekuwa mke wa kiongozi huyo Lipolelo mwaka wa 2017.

Waziri Mkuu wazamnai wa  Lesotho Thomas Thabane akiwa na  mkewe wa sasa  Maesaiah Thabane wakati kuapishwa kwake huko Maseru Juni 16 Juni 2017.
Waziri Mkuu wazamnai wa Lesotho Thomas Thabane akiwa na mkewe wa sasa Maesaiah Thabane wakati kuapishwa kwake huko Maseru Juni 16 Juni 2017. Photo: Samson Motikoe/AFP
Matangazo ya kibiashara

Waendesha mashtaka wameiambia mahakama iliyokuwa inasikiliza kesi hiyo jijini Maseru kuwa hatua hiyo imeafikiwa baada yao kushindwa kubaini aliko shahidi mkuu katika kesi hiyo.

Thabane, 83, alituhumiwa kwa kuwakodi watu iliwamuuwe Lipolelo mwezi Juni 2017, siku mbili kabla ya kuapishwa kuwa waziri mkuu.

Thabane na Lipolelo walisemekana kukabiliwa na kesi ya talaka dhidi yao wakati huo.

Waziri mkuu huyo wa zamani na mkewe wa sasa Maesaiah, ambaye alimuoa miezi miwili kupita baada ya mauaji ya Lipolelo wamekana kuhusika na njama hiyo.

Thabane alijiuzulu Mei 2020 kutokana na shinikizo za kumataka kufanya hivyo kwa sababu ya tuhuma zilizokuwa zinamkabili.

Uwamuzi wa kuondoa mashataka hayo dhidi yake umekuja ikiwa imepita wiki moja baada ya taifa hilo kutanagaza kuwa halitaanda uchaguzi mkuu wa mwezi Oktoba.

Polisi nchini humo ilimtuhumu Thabane kwa kuwalipa watu malipo ya awali ya $24,000 iliwamuwe mkewe.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.