Pata taarifa kuu
LESOTHO-SIASA-HAKI

Waziri mkuu wa Lesotho ajiuzulu kufuatia kashfa ya mauaji ya mke wake

Waziri mkuu wa Lesotho Thomas Thabane hatimaye ametangaza kuwa ataachia ngazi kwenye wadhifa wake baad ya miezi kadhaa ya maamdamano na vurugu kufuatia kashfa ya mauaji ya mke wake mkubwa.

Waziri Mkuu Thomas Thabane (katikati) na mkewe Maesaiah Thabane, hapa wakiambatana na Mfalme wa Lesotho Letsie III (kulia), huko Maseru, Juni 26, 2017.
Waziri Mkuu Thomas Thabane (katikati) na mkewe Maesaiah Thabane, hapa wakiambatana na Mfalme wa Lesotho Letsie III (kulia), huko Maseru, Juni 26, 2017. SAMSON MOTIKOE / AFP
Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo Bw Thabane, mwenye miaka 80, hakusema lini atatekeleza uamuzi huo wa kujiuzulu, lakini tayari chama chake cha ABC (All Basotho Convention) kimetangaza kwamba waziri mkuu mpya ataapishwa siku ya Jumatano.

Bwana Thabane anasisitiza kuwa shutuma dhidi yake hazina msingi wowote akidai kuwa zinachochewa kisiasa.

Lipolelo Thabane, 58, mkwe mkubwa Thomas Thabane, aliuawa Juni 14, 2017 alipokuwa anarudi nyumbani kwa gari huko Maseru, mji mkuu wa Lesotho. Siku mbili baadaye, mumewe, Thomas Thabane aliteuliwa rasmi kuwa Waziri Mkuu wa Lesotho.

Siku chache baadaye Thomas Thabane alionekana akifuatana kimapenzi na Maesaiah, ambaye baadaye alimuoa na kuwa mke wake wa pili.

Uchunguzi kuhusu mauaji ya Lipolelo Thabane ulisitishwa kwa kipindi cha miaka mbili. Mapema mwezi Februari 2020, mke mpya wa Waziri Mkuu alishtakiwa rasmi kwa mauaji ya mke mwenza. Ijumaa wiki hii ni zamu ya Waziri Mkuu Thomas Thabane kusikilizwa kuhusu mauaji hayo.

Thomas Thabane alipoteza wingi wa viti bungeni wiki iliyopita baada ya muungano unaomuunga mkono kugawanyika na serikali mpya inatarajiwa kushika usukani Ijumaa

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.