Pata taarifa kuu
DJIBOUTI-UFARANSA

Rais wa Djibouti Ismael Omar Guelleh akutana kwa mazungumzo na Emmanuel Macron

Rais wa Djibouti Ismael Omar Guelleh yuko ziarani jijini Paris tangu alhamisi wiki hii. Baada ya kukutana na wafanyabiashara wakuu wa Ufaransa na wajumbe wa Bunge la Seneti siku moja kabla, anatarajiwa kula chakula cha mchana na rais Emmanuel Macron.

Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron.
Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron. Photo by Ludovic Marin, Pool via AP
Matangazo ya kibiashara

Viongozi hawa wawili watajaribu kuziungumzia kuhusu makubaliano ya ushuru kati ya nchi hizo mbili, uwekezaji wa Ufaransa nchini Djibouti, na suala la kurejelea upya makubaliano ya ulinzi.

Rais Ismael Omar Guelleh alitarajiwa kuzuru Ufaransa kwa muda mrefu, lakini ziara yake ilicheleweshwa na mvutano kuhusu hatima ya kambi ya kikosi cha wanamaji cha Ufaransa katika eneo moja ambalo serikali ya Djibouti inataka kutumia kwa mambo mengine.

Kama sehemu ya makubaliano ya ulinzi ambayo yanatarajiwa kurejelewa upya kabla ya kumalizika muda wake, Paris inataka kambi hiyo iendelee kuwepo katika eneo hilo, lakini Djibouti inataka

kufanya eneo hilo kuwa la kibiashara. Haijulikani kwamba maelewano yatapatikana kati ya nchi hizi mbili kuhusiana na suala hilo.

Lakini Rais Guelleh pia anakuja kuzungumza juu ya uwekezaji wa Ufaransa nchini mwake. Mkataba na mkoa wa Provence-Alpes-Côte d´Azur (PACA) unakaribia kusainiwa, na vile vile na kampuni ya umeme ya Engie.

Mkutano huu kati ya marais hawa wawili pia unafanyika katika hali ngumu ya kisiasa. Djibouti imejiondoa kwenye mzozo mbaya wa jirani yake Ethiopia, huko Tigray, lakini iimeihusisha hasimu wake Eritrea.

Hayo yanajiri wakati rais Guelleh anawania muhula wa tano katika uchaguzi wa urais uliopangwa kufanyika mwezi wa Aprili 2021, na anakikabiliwa na upinzani ambao hivi karibuni ulitangaza kuwa utasusia uchaguzi huo. Wakati huo huo upinzani ulitoa wito kwa washirika wa kigeni wa Djibouti kwa msaada, ili kuepuka vurugu kubwa katika nchi hii ya kimkakati ya Afrika.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.