Pata taarifa kuu
SIASA-HAKI

Congo-Brazzaville: Nani atakuwa kiongozi mpya wa upinzani?

Baada ya uchaguzi wa wabunge na muundo wa afisi mpya ya Bunge, swali moja bado halijatatuliwa. Nani atakuwa kiongozi mpya wa upinzani? Bado hajateuliwa hadi sasa, miezi miwili baada ya uchaguzi wa wabunge, huku vyama vya Pan-African Union for Social Democracy na Union of Humanist Democrats, vyama viwili vya upinzani vilivyopata idadi sawa ya wabunge, 7 kila kimoja, kikitaka kuchukuwa nafasi hiyo.

Makao makuu ya Baraza la Wawakilishi nchini Congo-Brazzaville.
Makao makuu ya Baraza la Wawakilishi nchini Congo-Brazzaville. assemblee-nationale.cg
Matangazo ya kibiashara

Baada ya kuunda makundi yao ya bunge wiki iliyopita, vyama vya UPADS na UDH-Yuki bado havijawekwa kwenye nafasi ya kiongozi wa upinzani, nafasi ambayo inashikiliwa hadi sasa na Pascal Tsaty Mabiala wa chama cha UPADS.

"Kimantiki, anapaswa kuteuliwa tena kwenye nafasi hiyo au kushikilia nafasi hiyo kwa kuzingatia matokeo ya uchaguzi wa wabunge wa 2017 ambapo chama cha UPADS kilikuwa na maafisa wanane waliochaguliwa", chanzo kutoka chama hicho kimebaini.

Pia mnamo 2017, chama cha UDH-Yuki kilikuwa bado hakijapata hati ya kukubaliwa kama chama kutoka Wizara ya Utawala wa Wilaya, kwa hivyo hakikutambuliwa rasmi kama chama cha kisiasa.

"Wakati wa uchaguzi wa wabunge wa 2022, chama cha UDH-Yuki kiliona wabunge wake wakichaguliwa kwa kura nyingi, hasa katika mji wa Brazzaville, tofauti na chama cha UPADS ambacho kilipata viti kadhaa katika mikoa pekee. Kiongozi wa upinzani lazima awe ni kutoka chama cha UDH, "anasema afisa wa chama hiki kilichoundwa na hayati Guy-Brice Parfait Kolélas.

Swali linabaki wazi bila shaka, lakini kwa kukosekana kwa maafikiano, kiongozi anayeondoka anaweza kuendelea kushikilia nafasi hiyo, kulingana namtaalam wa masuala ya Katiba.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.