Pata taarifa kuu
CONGO BRAZZAVILLE

Congo-Brazzaville: Guy-Brice Parfait Kolélas bado hajazikwa miezi mitano baada ya kifo chake

Mpinzani huyo wa Congo alifariki dunia siku moja baada ya uchaguzi wa urais Machi 21, 2021, ambapo alikuwa mgombea katika uchaguzi huo. Lakini kutokubaliana ndani ya familia yake, kuhusiana na tarehe ya kifo chake hasa, ndio sababu kuu ya kucheleweshwa kwa taratibu za mazishi.

Guy-Brice Parfait Kolélas alifariki dunia siku moja baada ya uchaguzi wa urais Machi 21, ambapo alikuwa mgombea.
Guy-Brice Parfait Kolélas alifariki dunia siku moja baada ya uchaguzi wa urais Machi 21, ambapo alikuwa mgombea. AFP - MARCO LONGARI
Matangazo ya kibiashara

Katika siku za hivi karibuni, tarehe ya mazishi ya Guy-Brice Parfait Kolélas ilitajwa kwenye mitandao ya kijamii: Septemba 10. Lakini kutangazwa kwa tarehe hiyo kulibuwa maswali mengi kwa upande umoja wa familia ya mwanasiasa huyo wa Congo inayoishi Paris ambayo, inapingana na tarehe hiyo, kulingana na taarifa.

Kulingana na uchunguzi na vipimo vilivyofanyiwa maiti, alifariki dunia kutokana na Covid-19  Machi 22. Lakini kulingana na wengine, alifariki dunia Machi 21, siku ya uchaguzi wa urais, na kutilia shaka juu ya ukweli wa uchaguzi huo. Kwa hivyo familia inataka tarehe hii irekebishwe rasmi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.