Pata taarifa kuu

Congo-Brazzaville: Waziri Mkuu wa zamani, Clément Mouamba, afariki kwa Covid-19

Waziri Mkuu wa Congo-Brazzaville kati ya 2016 na Mei 2021, Clément Mouamba, alifariki Ijumaa, Oktoba 29, kwa Covid-19 huko Paris, ambapo alikuwa amesafirishwa kwa matibabu, zaidi ya wiki mbili zilizopita. Alikuwa na umri wa miaka 78.

Clément Mouamba, Waziri Mkuu wa Congo-Brazzaville kuanzia mwezi Aprili 2016 hadi mwezi Mei 2021.
Clément Mouamba, Waziri Mkuu wa Congo-Brazzaville kuanzia mwezi Aprili 2016 hadi mwezi Mei 2021. © STR / AFP
Matangazo ya kibiashara

Chama cha Congolese Labour (PCT), chama tawala ambacho Clément Mouamba alikuwa mfuasi wake, kilitangaza kifo chake Ijumaa, Oktoba 29. Waziri Mkuu wa sasa, Anatole Collinet Makosso, alitoa rambirambi kwa familia yake. "Ninapoteza mtu muhimu," alisema. Clément Mouamba alikua Waziri Mkuu baada ya uchaguzi wa urais wa mwaka 2016 uliokuwa na ushindani mkubwa.

Mchumi huyu, kada wa Benki ya Mataifa ya Afrika ya Kati (BEAC), alijitolea kurekebisha mizani ya uchumi mkubwa. Muda mfupi kabla, alikuwa amejiunga na chama tawala baada ya kufukuzwa kutoka chama kikuu cha upinzani cha Pan African Union for Social Democracy (UPADS) kwa kukubali kushiriki katika mazungumzo ya kitaifa yaliyopelekea mabadiliko ya katiba.

Clément Mouamba pia alihudumu katika utawala wa Profesa Pascal Lissouba, rais wa kwanza kuchaguliwa nchini Congo, ambaye alikuwa Waziri wa Fedha kati ya mwaka 1992 na 1993. Tangu mwaka 2017, alikuwa pia mbunge wa jimbo la Sibiti, kusini mwa Congo, mji alikozaliwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.