Pata taarifa kuu
GAMBIA- SIASA.

Gambia: Majasusi wa zamani wahukumiwa kifo kwa kuhusishwa na mauaji

Mahakama nchini Gambia imetoa hukumu ya kifo dhidi ya majasusi watano wa zamani baada ya kuwakuta na hatia ya kuhiska na mauaji ya mwanaharakati wa kisiasa wakati wa utawala wa dikteta Yahya Jammeh.

Yahya Jammeh aliyekuwa rais wa Gambia.
Yahya Jammeh aliyekuwa rais wa Gambia. GRTS - Gambia Radio and Television Services/AFP/File
Matangazo ya kibiashara

Jaji wa mahakama kuu Kumba Sillah-Camara, katika hukumu yake amemkuta mkuu wa zamani wa Intelijensia nchini humo, Yankuba Badjie, na makosa ya kumuua Ebrima Solo Sandeng,mwanasiasa wa chama upinzani cha United Democratic Party,mwaka wa  2016.

Wengine waliokutwa na hatia ni pamoja na aliyekuwa mkuu wa mipango katika kitengo cha Intelijensia wakati huo Sheikh Omar Jeng, Babucarr Sallah, Lamin Darboe na Tamba Mansary.

Sandeng, alikamatwa wakati wa maandamano dhidi ya utawala wa Jammeh ya Aprili 2016. Alifariki baada ya kuwa kizuizini kwa siku mbili kutokana na majeraha aliopata baada ya kupigwa na kuteswa mikononi mwa vyombo vya usalama.

Kifo chake kilisababisha maandamano makubwa yalioangusha utawala wa Jammeh,aliyekuwa ameongoza taifa hilo la Afrika magharibi kwa miaka 22.

Haruna Susso, afisa mwengine wa intelijensia na Lamin Sanyang, mhudumu wa afya hawakutwa na hatia katika kesi hiyo.

Kesi hiyo ilioanza mwaka wa 2017 ilikuwa kesi peke ambao ilikuwa ingali inasikilizwa na mahakama ya nchini humo kufuatia tuhuma za visa vya uhalifu wa kibinadamu wakati wa utawala wa Jammeh.

Hukumu hii inakuja wakati huu Jammeh akiwa mafichoni nchini Equatorial Guinea, aliko kimbilia usalama wake mwaka wa 2017 baada ya kupoteza katika uchaguzi mkuu wa urais wa mwaka 2016 dhidi ya Adama Barrow.

Mwaka wa 2017 Barrow alifanya mageuzi katika idara ya intelijensia ambapo ibadilishwa jina kutoka kwa NIA ambapo sasa inajulikana kama (SIS).

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.