Pata taarifa kuu
SOMALIA-DIPLOMASIA

Waziri Mkuu wa Somalia aagiza kutimuliwa kwa mwakilishi wa AU, rais apinga

Waziri Mkuu wa Somalia Mohamed Hussein Roble siku ya Alhamisi aliagiza kufukuzwa kwa mwakilishi wa Umoja wa Afrika nchini humo, jambo lililozua mzozo mpya na Rais Farmajo ambaye alielezea uamuzi huo kuwa "ni kinyume cha sheria".

Rais wa Somalia Mohammed Abdullahi Mohammed Farmajo na Waziri mkuu Mohamed Hussein Roble.
Rais wa Somalia Mohammed Abdullahi Mohammed Farmajo na Waziri mkuu Mohamed Hussein Roble. © Caasimada Online
Matangazo ya kibiashara

Wawili hao wanakinzana mara kwa mara katika miezi ya hivi karibuni, na kuchochea mzozo wa kisiasa ambao unachelewesha kuandaa uchaguzi wa urais unaotarajiwa kwa zaidi ya mwaka mmoja katika nchi hii isiyo na utulivu katika Pembe ya Afrika, iliyokumbwa kwa miaka 15 na uasi wa Kiislamu wa Al Shabab. .

Ofisi ya Roble imesema katika taarifa yake Alhamisi asubuhi kwamba ilikuwa imemtangaza Francisco Madeira kwamba" haina imani naye tena kwa kujihusisha na vitendo visivyoendana na hadhi yake kama mwakilishi wa Tume ya Umoja wa Afrika", ikiagiza kuondoka Somalia ndani ya saa 48.

Taarifa hiyo haikutoa maelezo yoyote kuhusu sababu za hatua hiyo inayomlenga Bw Madeira, mwanadiplomasia wa Msumbiji ambaye amekuwa mwakilishi maalum wa Mkuu wa Kamisheni ya AU nchini Somalia tangu mwaka 2015.

Saa chache baadaye, Rais Mohamed Abdullahi Mohamed, anayejulikana zaidi kwa jina la Farmajo, alipinga tamko hili.

Rais "hajapokea malalamiko yoyote ya kuingiliwa kwa mamlaka yake na hakubaliani na hatua zozote zisizo halali dhidi ya Balozi Francisco Madeira," taarifa kutoka ofisi ya rais imesema.

Ikikumbukwe kwamba "Farmajo ndiye mlinz na mdhamini wa uhuru wa nchi", ofisi ya rais inabaini kwamba imemwagiza Waziri wa Mambo ya Nje "kuwasilisha msamaha wa serikali ya shirikisho kwa Umoja wa Afrika kwa uamuzi usio halali na wa kizembe kwa uidara ambayo haijaidhinishwa " kufanya hivyo.

Umoja wa Afrika upo nchini Somalia kupitia kikosi cha kulinda amani, ambacho kilitumwa mwaka 2007 chini ya jina la Misheni ya AU nchini Somalia (AMISOM).

Wiki iliyopita, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilipiga kura kwa kauli moja kurefusha kikosi hiki hadi mwisho wa mwaka 2024, katika ujumbe ulioundwa upya na kuitwa Misheni ya Mpito ya Somalia (ATMIS).

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.