Pata taarifa kuu

Somalia: Washirika wa kimataifa wataka kukamilishwa kwa mchakato wa Bunge

Jumuiya ya Kimataifa, inawataka wanasiasa nchini Somalia kutumia njia ya mazungumzo ili kumaliza mvutano wa kisiasa nchini humo, baada ya zoezi la kuwachagua wabunge kutomalizika Machi tarehe 15 na hivyo, kuahirishwa mpaka mwisho wa mwezi. 

Somalia inaendelea kuathirika kutokana na mizozo ya kisiasa isiyoisha.
Somalia inaendelea kuathirika kutokana na mizozo ya kisiasa isiyoisha. REUTERS - FEISAL OMAR
Matangazo ya kibiashara

Aidha, mataifa ya kigeni  yanataka asilimia 30 ya viti vitengewe wanawake kama ambavyo inavyotakiwa. 

Kutomalizika kwa zoezi hilo, kunamaanisha kuwa zoezi la kumchagua rais pia litacheleweshwa. 

Kwa mara ya tatu katika muda wa miezi mitatu, tarehe ya mwisho ya uchaguzi wa wabunge wote wa baraza Wawakilisi hukufanyika tena Jumatano hii, Machi 16, 2022. Majimbo matatu ya shirikisho bado hayajaweza kuchagua wawakilishi wao. Kwa hivyo tume inayosimamia mchakato wa uchaguzi imeweka makataa mapya. Lakini uchaguzi huu muhimu kwa nchi hii bado umegubikwa na sintofahamu nyingi.

Bunge la Somalia bado lina upungufu wa wabunge 39, wawakilishi 39 wa majimbo ya Jubaland, Punland na Hirshabelle. Lakini hakuna dalili kwamba majimbo haya matatu yataweza kuwateua wajumbe wao kabla ya Machi 31 na kwamba kuapishwa kwao kunaweza kufanyika Aprili 14, kama kamati ya utekelezaji wa uchaguzi sasa inapanga, baada ya tarehe ya mwisho kupita siku ya Jumatano bila kutangazwa tarehe mpya ya uchaguzi.

Puntland imetangaza kuwa uchaguzi wake utafanyika siku ya Ijumaa, lakini bado kuna mvutano. Hasa kuhusu uungwaji mkono au la kuhusu kwa rais anaye maliza muda wake, Mohamed Abdullahi Mohamed anayejulikana kama "Farmajo" kuongezwa muhula wa kuitawala nchi hiyo, ameelezea mwandishi wa habari wa Somalia.

Wikihii Marekani ilitangaza kuongeza idadi ya maafisa wa Somalia iliyowawekea vikwazo vya kutosafiri katika nchi yake, kwa kuendelea kurudisha nyuma mchakato wa kidemokrasia katika taifa hilo la pembe ya Afrika.

Hatua hii imekuja baada ya Kamati ya Uchaguzi siku ya Jumatano kuahirisha kumalizika kwa zoezi la kuwachagua wabunge, mpaka mwisho wa mwezi huu, na hivyo kuchelewesha zoezi la kumchagua rais.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.