Pata taarifa kuu
SOMALIA-UCHAGUZI

Somalia yashindwa kufanikisha zoezi la uchaguzi wa wabunge

Nchini Somalia, majimbo mawili bado hayajafanikiwa kumaliza uchaguzi wa wawakilishi wao bungeni, licha ya siku ya mwisho kuwa hivi leo. 

Uchaguzi nchini Somalia ulikuwa umepangwa kufanyika kabla ya Desemba 31.
Uchaguzi nchini Somalia ulikuwa umepangwa kufanyika kabla ya Desemba 31. REUTERS/Feisal Omar
Matangazo ya kibiashara

Mpaka siku ya mwisho ambayo uchaguzi huo ulipaswa kufanyika, ni majimbo sita kati ya nane ndio yaliyomaliza zoezi la kuwachagua wawakilishi wao. 

Asilimia 90 ya viti bungeni ambavyo ni sawa na 275 vimeshajazwa isipokuwa 16 kutoka majimbo hayo mawili katika eneo la Kusini mwa Jubaland, kuelekea kuapishwa mwezi ujao. 

Mvutano wa kisiasa unaelezwa kuwa sababu kuu ya zoezi hili kutokamilika kama ilivyopangwa na hivi kurudisha nyuma mchakato wa bunge kumchagua rais. 

Nchini Somalia kwa zaidi ya miaka 50 sasa, wananchi hawajapata fursa ya kupiga kura moja kwa moja kumchagua rais badala yake anachaguliwa na wabunge, ambao huchaguliwa  na viongozi wa koo  na mashirika ya kiraia mbalimbali nchini humo. 

Jumuiya ya Kimataifa imesikitishwa na Somalia kutofanikiwa kufanikisha zoezi la uchaguzi nchini humo tangu mwezi Februari na hata baadhi ya watu nchini humo wamewekewa vikwazo na serikali ya Marekani kwa kuchelewesha Uchaguzi huo 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.