Pata taarifa kuu
ETHIOPIA-USALAMA

Ethiopia: Waasi wa Tigray wakubali kanuni ya ‘kusitisha uhasama’

Saa chache baada ya serikali ya Ethiopia kutangaza "usitishwaji wa vita ili kuruhusu misaada ya kibinadamu kuwafikia watu katika jimbo la Tigray" , Kaskazini mwa nchi hiyo, waasi wa Tigray wa TPLF nao wameahidi kusitisha mapigano. Ishara nzuri, lakini ambayo haimaanishi kurejea mara moja kwa misaada ya kibinadamu katika eneo hilo.

Basi lililochomwa moto kando ya barabara katika eneo la Tigray.
Basi lililochomwa moto kando ya barabara katika eneo la Tigray. © RFI/Sébastien Nemeth
Matangazo ya kibiashara

Jibu la TPFL ni hatua katika mwelekeo sahihi. Katika taarifa yao kwa vyombo vya habari iliyotolewa Ijumaa hii asubuhi, waasi wa Tigray wanafanya kwa upande wao "kutekeleza" makataba wa "kusitisha uhasama, na kutekelezwa mara moja", kwa kujibu mapatano "yasiyo na kikomo" yaliyotangazwa Alhamisi na Addis Ababa. Kauli zinazodaiwa mara ya kwanza kuruhusu kurejeshwa kwa misaada ya kibinadamu kwa Tigray, chini ya vizuizi tangu Desemba mwaka jana.

Lakini bado kuna maswali magumu ya kutatua. Mbali na kusitishwa kwa mapigano, Addis Ababa inatarajia kundi la waasi wa Tigray kuondoa wanajeshi wake katika eneo jirani la Afar. Hayo yamethibitishwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ethiopia.

Hata hivyo, TPFL haijibu hoja hii katika taarifa yake kwa vyombo vya habari. Kinyume chake, inaomba serikali ya Ethiopia "kuchukua hatua madhubuti kuwezesha ufikiaji usio na kikomo kwa misaada katika jimbo la Tigray" na inaonekana kufanya hili kuwa sharti kabla ya kujiondoa, kulingana na vyanzo vya kidiplomasia. Hata hivyo tangu mwezi Desemba mwaka jana, kwa matumaini ya msaada wa haraka wa kibinadamu kwa jimbo la Tigray, waasi wa TPLF walirudi nyuma, lakini msaada huo haufika.

Tangu mwezi Desemba 15 mwaka 2021, malori ya Tume ya Umoja wa Mataifa linalohusika na misaada ya kibinadamu OCHA, ilisitisha shughuli za kupeleka misaada kwa sababu za kiusalama, huku Marekani ikiilaumu serikali ya Ethiopia kwa kukwamisha hatua hiyo.

Vita katika Jimbo la Tigray lililoanza mwezi Novemba mwaka 2020 vimesababisha maafa makubwa na watu wengine Laki Nne kusalia wakimbizi katika jimbo hilo na wengine kukilbilia nchi jirani kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.