Pata taarifa kuu

Serikali ya Ethiopia yatangaza 'makubaliano ya kuruhusu misaada ya kibinadamu'

Serikali ya Ethiopia siku ya Alhamisi imetangaza "makubaliano yasio na kikomo ya kurhusu misaada ya kibinadamu" katika mzozo wake na waasi wa Tigray, ili kuruhusu "kuingia kwa misaada ya kibinadamu kwa wale wanaohitaji" katika eneo hili la kaskazini mwa nchi linalotishiwa na njaa.

Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed, Oktoba 4, 2021.
Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed, Oktoba 4, 2021. AFP - AMANUEL SILESHI
Matangazo ya kibiashara

Makubaliano hayo "yanatumika mara moja", serikali ya Waziri Mkuu Abiy Ahmed imesema katika taarifa, ikielezea uamuzi wake wa "haja ya kuchukua hatua muhimu kuokoa maisha ya raia".

Hata hivyo, "ahadi iliyotolewa na serikali ya Ethiopia inaweza tu kuwa na matokeo chanya yanayotarajiwa (...) ikiwa upande mwingine utafanya vivyo hivyo", ameongeza, akitoa wito kwa waasi wa Tigray "kujiepusha na kitendo chochote kipya cha uchokozi na kujiondoa katika maeneo wanayomiliki katika mikoa jirani ya Tigray". Waasi wa Tigray hawakujibu mara moja tangazo hili.

Vikosi vinavyounga mkono serikali na waasi kutoka Tigray vimekuwa vikipambana kaskazini mwa Ethiopia tangu mwezi wa Novemba 2020 ambapo Abiy Ahmed, mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel mwaka uliotangulia, alituma jeshi la shirikisho kuwaondoa mamlakani viongozi katika eneo lililokuwa likitawaliwa na chama cha Tigray People's Liberation Front TPLF), ambacho kilikuwa kinapinga mamlaka yake kwa miezi kadhaa.

Wakiwa wameshindwa haraka, vikosi vya waasi wa TPLF wakati huo, mwaka 2021, waliudhibiti tena mji wa Tigray na mzozo huo umeenea katika mikoa jirani ya Amhara na Afar.

Uingereza na Canada zimekaribisha tangazo la makubaliano haya, na kutoa wito kwa pande zote kuheshimu. "Uingereza inakaribisha uamuzi wa serikali ya Ethiopia wa kutangaza usitishaji wa ukiukaji wa haki za kibinadamu kwa muda usiojulikana na kuhakikisha ufikiaji usiozuiliwa wa msaada kwa Tigray. Tunatoa wito kwa viongozi wa Tigray kufanya hivyo," umesema Ubalozi wa Uingereza nchini Ethiopia kwenye Twitter.

Ubalozi wa Canada nchini Ethiopia na Djibouti umepongeza "habari njema, kwani msaada unahitajika kwa dharura kaskazini mwa Ethiopia." Wanadiplomasia wa kigeni wakiongozwa na Olusegun Obasanjo, mjumbe maalum wa Umoja wa Afrika katika Pembe ya Afrika, wamekuwa wakijaribu kwa miezi kadhaa kupata mazungumzo ya amani, huku kukiwa na maendeleo madogo yanayoonekana.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.