Pata taarifa kuu
MALI-MAZUNGUMZO

ECOWAS kuijadili Mali, Goïta asusia mkutano

Wakuu wa nchi za Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS) wanakutana Ijumaa hii, Machi 25 kuanzia saa kumi na moja jioni saa za Afrika Mashariki mjini Accra, Ghana, katika kikao kisichokuwa cha kawaida, kujadili mustakabili wa  kisiasa nchini Mali, mkutano ambao kiongozi wa kijeshi Assimi Goïta, hatohudhuria.

Assimi Goïta, rais wa Baraza la Kitaifa la Wokovu wa Watu (CNSP) nchini Mali, wakati wa mkutano wa kilele wa ECOWAS mjini Accra, Septemba 15, 2020.
Assimi Goïta, rais wa Baraza la Kitaifa la Wokovu wa Watu (CNSP) nchini Mali, wakati wa mkutano wa kilele wa ECOWAS mjini Accra, Septemba 15, 2020. © Nipah Dennis / AFP
Matangazo ya kibiashara

Mkutano huu unafanyika siku chache baada ya mpatanishi wa Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS), rais wa zamani wa Nigeria Goodluck Jonathan kutamatisha ziara yake jijini Bamako wiki iliyopita, ambako alishindwa kuafikiana na serikali ya nchi hiyo kuhusu mapendekezo ya Jumuiya hiyo.

Miongoni mwa mapendekezo hayo ikiwa ni pamoja na kutangazwa kwa tarehe ya uchaguzi ujao ili kuruhusu kurejea kwa utawala wa kiraia, baada ya uongozi wa mpito kusema uchaguzi unaweza kufanyika baada ya miaka mitano.

Hata hivyo utawala wa kijeshi unaoongozwa na Assimi Goita umesusia mkutano huu kwa kile unachodai kwamba baadhi ya masharti yaliyowasilishwa mbele ya ujumbe wa ECOWAS uliotembelea Mali hivi karibuni hayakufanyiwa kazi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.