Pata taarifa kuu
MALI-HAKI

Mahakama ya WAEMU yasitisha vikwazo vya kiuchumi vya Afrika Magharibi dhidi ya Mali

Uamuzi ambao unakuja wakati mkutano mpya wa kilele wa ECOWAS, Jumuiya ya Mataifa ya Afrika Magharibi, kuhusu hali nchini Mali, utafanyika kesho, Ijumaa. Mkutano ambao rais wa mpito, Assimi Goïta, amealikwa.

Mji mkuu wa Mali, Bamako, kando ya Mto Niger, pamoja na jengo la BCEAO, Benki Kuu ya Mataifa ya Afrika Magharibi, likiwa mbele (kwenye picha).
Mji mkuu wa Mali, Bamako, kando ya Mto Niger, pamoja na jengo la BCEAO, Benki Kuu ya Mataifa ya Afrika Magharibi, likiwa mbele (kwenye picha). Getty Images/John Elk
Matangazo ya kibiashara

Habari hiyo imewasilishwa na mmoja wa mawakili wa serikali ya Mali na kuthibitishwa na chanzo kutoka jumuiya hiyo siku ya Alhamisi Machi 24. Mahakama ya WAEMU, Muungano wa Fedha wa Afrika Magharibi, imefahamisha serikali ya Mali kuhusu uamuzi wake wa kusimamisha vikwazo vinavyoathiri Bamako.

Ushindi huo sio kamili, lakini ni jambo lisilopingika kwa mamlaka ya mpito ya Mali ambayo mara kwa mara imelaani vikwazo vya kiuchumi na kifedha vilivyowekwa dhidi ya Mali tangu Januari 9. Kama ukumbusho, kundi la mawakili waliwasilisha malalamiko yao mbele ya Mahakama, Februari 15, dhidi ya vikwazo vilivyochukuliwa Januari 9 na viongozi wa kanda hiyo, kufuatia tangazo la kuongezwa kwa muda wa kipindi cha mpito. Rufaa ya kwanza iliomba kufutwa kwa vikwazo hivyo, na rufaa ya pili, iliomba kusimamishwa hatua zotezilizochukuliwa dhidi ya Mali  kwa sababu ya athari zake kwa raia.

Mkutano wa kilele wa ECOWAS Ijumaa hii

Kama Mahakama ya Haki ya WAEMU haikupata uharamu wake, hata hivyo ilisikia hoja kwamba athari yake ilikuwa "ya chuki kubwa" sio tu kwa serikali ya Mali, lakini kwa Wamali wenyewe. Kwa muda wa miezi miwili na nusu, mahusiano yote ya kibiashara na kifedha ya Mali na nchi za ECOWAS yamepigwa marufuku, jambo ambalo limepelekea serikali kushindwa kulipa katika soko la fedha, na kupanda kwa bei nchini humo licha ya kufutiwa ushuru kwa mahitaji ya kimsingi au dawa.

Kwa hivyo Mahakama ya Haki ya WAEMU haifuti vikwazo hivyo lakini inaomba ECOWAS kusitisha utekelezaji wake. Mkutano usio wa kawaida wa Jumuiya ya Kiuchumi ya nchi za Afrika Magharibi umepangwa kufanyika kesho, Ijumaa, ambapo rais wa mpito wa Mali, Kanali Assimi Goïta, amealikwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.