Pata taarifa kuu

ECOWAS kuijadili Mali siku chache baada ya matangazo ya RFI na France 24 kusitishwa

Jumuiya ya kiuchumi ya nchi za Afrika Magharibi ECOWAS, itakuwa na kikao kisichokuwa cha kawaida cha viongozi wa nchi hizo siku ya Ijumaa, kujadili hali ya kisiasa nchini Mali.

Baadhi ya viongozi wa ECOWAS wakiwa kwenye kikao cha kawaida cha 60  mjini Abuja.
Baadhi ya viongozi wa ECOWAS wakiwa kwenye kikao cha kawaida cha 60 mjini Abuja. © Nigeria presidency
Matangazo ya kibiashara

Kikao hicho kitafanyika jijini Accra nchini Ghana, wiki moja baada ya mjumbe wa ECOWAS rais wa zamani wa Nigeria Goodluck Jonathan kuzuru jijini Bamako na kuondoka bila ya kuafikiana na kiongozi wa kijeshi ni lini uchaguzi utafanyika.

Haijafahamika vema iwapo kiongozi wa kijeshi Kanali Assimi Goita ambaye aliingia madarakani baada ya mapinduzi ya kijeshi atahudhuria kikao hicho.

Uongozi wa kijeshi umeshindwa kuandaa uchaguzi kama inavyoshinikizwa na Jumuiya ya Kimaytaifa ili kurejesha uongozi wa kiraia na badala yake unataka uchaguzi huo kufanyika baada ya miaka mitano.

Mwezi Januari, Jumuiya ya ECOWAS iliiwekea vikwazo vya kiuchumi nchi ya Mali na kufunga mipaka yake, kuendeleza shinikizo kwa nchi hiyo kurejesha uongozi kwa raia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.