Pata taarifa kuu

Njaa yatishia watu milioni 13 katika Pembe ya Afrika

Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani limesema kwamba watu milioni 13 katika Pembe ya Afrika wana njaa, likitoa wito wa usaidizi wa haraka ili kuepusha kujirudia kwa njaa iliyoua mamia ya maelfu ya watu muongo mmoja uliopita.

 Wanawake kutoka jamii ya Turkana wakisubiri msaada wa chakula huko Kalok Tonyang katika wilaya ya Turkana kaskazini-magharibi mwa Nairobi, Agosti 9, 2011.
Wanawake kutoka jamii ya Turkana wakisubiri msaada wa chakula huko Kalok Tonyang katika wilaya ya Turkana kaskazini-magharibi mwa Nairobi, Agosti 9, 2011. Reuters/Kabir Dhanji
Matangazo ya kibiashara

Misimu mitatu ya mvua iliyofeli imesababisha hali ya ukame zaidi tangu miaka ya 1980, na utabiri wa mvua za chini ya wastani unatarajiwa kuongeza mateso katika miezi ijayo.

"Mazao yanaharibiwa, mifugo inakufa na njaa inazidi kuongezeka kutokana na ukame wa mara kwa mara unaoathiri Pembe ya Afrika," amesema Michael Dunford, mkurugenzi wa kikanda katika ofisi ya WFP katika kanda ya Afrika Mashariki.

Hali hizi zimepunguza mifugo, na kuwalazimu maelfu ya watu katika eneo ambalo wengi ni wakulima kukimbilia kwenye kambi za wkimbizi wa ndani.

"Hatujawahi kuona haya hapo awali, tunaona tu dhoruba zinazorusha vumbi kwa sasa. Tunaogopa kwamba zitatufunika sote na kuwa makaburi yetu," Mohamed Adem, raia wa Ethiopia, amesema kwenye video ya shirika la WFP.

Ethiopia, Kenya, Somalia na Eritrea

Picha zilizopigwa zaonyesha eneo kubwa la vumbi lilkitapakaa mizoga ya ng'ombe.

"Wakati haujadhibitiwa, kuna ukame mkubwa katika maeneo ya Somalia na sehemu za Oromia na majimbo ya eneo la Kusini," msemaji wa serikali Legesse Tulu ameliambia shirika la habari la Reuters. "Onyo la WFP kwa hiyo ni sahihi kabisa."

Ukame pia unaenea katika maeneo ya Kenya, kusini-kati mwa Somalia na Eritrea. Kati ya mwaka 2010 na 2012, karibu watu 250,000 walikufa kwa njaa nchini Somalia, nusu yao wakiwa watoto.

Mohamed Fall wa UNICEF, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, ameonya katika kikao cha kuelimishana kwamba watoto wengi watakufa au kupata madhara ya kiakili au kimwili ikiwa hatua za haraka hazitachukuliwa.

"Lazima tuchukue hatua sasa ili kuepusha janga," amesema kwa simu kutoka Nairobi, akiongeza kuwa watoto milioni 5.5 katika mataifa hayo manne kwa sasa wako katika hatari ya kupata utapiamlo mkali.

WFP, ambayo ilishinda Tuzo ya Amani ya Nobel mwaka 2020, inazindua mpango wake wa kusaidia Pembe ya Afrika wiki hii na inaomba dola milioni 327. UNICEF inaomba dola milioni 123.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.