Pata taarifa kuu
ETHIIOPIA-MAZUNGUMZO

Ethiopia: Waziri Mkuu atangaza uwezekano wa mazungumzo na TPLF

Nchini Ethiopia, Waziri Mkuu Abiy Ahmed amehutubia Baraza la Wawakilishi siku ya Jumanne na Jumatano. Zoezi la kuhalalisha hadharani kile anachokiona kama sera ya kutuliza uhasama wa kijamii, baada ya karibu miezi kumi na sita ya vita dhidi ya waasi wa Tigray. Wakati wa hotuba yake, ametaja uwezekano wa mazungumzo na kundi la waasi wa TPLF katika siku zijazo.

Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed mjini Addis Ababa, Oktoba 4, 2021.
Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed mjini Addis Ababa, Oktoba 4, 2021. AFP - AMANUEL SILESHI
Matangazo ya kibiashara

Siku mbili mbele ya wabunge, siku mbili kuelezea msimamo wa sasa wa serikali ya Ethiopia, katika mazingira mapya na yanayobadilika sana. Ilikuwa ni lazima kwa Abiy Ahmed kujulisha mtazamo wake wa sasa kuhusu nchi yake.

Ikiwa, katika siku ya kwanza, alikaribisha kuinuka kwa uchumi baada ya kupunguwa kwa mapigano, na kutangaza ubinafsishaji mpya, siku ya pili ilikuwa fursa ya kuweka rekodi sawa juu ya matarajio ya amani. Kuhusu, kwa mfano, kufanya mazungumzo na adui yake, TPLF, ameeleza kuwa sivyo ilivyo kwa sasa, lakini “hii haijatenga uwezekano wa kufanya mazungumzo”.

“Kuleta Amani ya Kudumu”

Akiwa amekabiliwa na sintofahamu hata katika kambi yake mwenyewe kuhusu kuachiliwa kwa wafungwa wa kisiasa hivi majuzi, alieleza kwamba kumechochewa na tamaa ya "kuleta amani ya kudumu, kwa kuzingatia hali ya jumla ya wafungwa, na kuimarisha ushindi wa kijeshi dhidi ya waasi wa TPLF, " amesema.

Hata hivyo Abiy Ahmed ameomba kwamba "mazungumzo ya kitaifa", ambayo alianzisha wiki hii, yaliyokosolewa na wanasiasa mbalimbali nchini Ethiopia, "yachukuliwe kwa uzito". Jumatano hii asubuhi, amekutana pia na viongozi wa chama chake, ili kujaribu kutuliza mvutano kuhusiana na masuala yote haya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.