Pata taarifa kuu
CAR-USALAMA

CAR: Walinda amani wanne kutoka Ufaransa wakamatwa Bangui

Nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, wanajeshi wanne wa Ufaransa kutoka Minusca, ujumbe wa Umoja wa Mataifa katika Jamhuri ya Afrika ya Kati, walikamatwa na jeshi la polisi Jumatatu, Februari 21, jioni katika uwanja wa ndege wa Bangui. Mara moja, picha zao zilirushwa kwenye mitandao ya kijamii zikiambatana na shutuma za "jaribio la kumuua" rais wa Afrika ya Kati. Ubalozi wa Ufaransa na Umoja wa Mataifa wamelaani  "habari za uongo zisizo na msingi".

Gari la Minusca linashika doria Bangui mnamo Desemba 22, 2020.
Gari la Minusca linashika doria Bangui mnamo Desemba 22, 2020. AFP - ALEXIS HUGUET
Matangazo ya kibiashara

Jenerali Marchenoir, Mkuu wa vikosi vya Minusca, alikuwa anaondoka kuelekea Paris wakati askari wanne wa Ufaransa kutoka kikosi chake cha ulinzi walikamatwa na kisha kuingizwa kwenye gari la askari jeshi wa Jamhuri ya Afrika ya Kati. Uwanja wa ndege wa Bangui wakati huo ulikuwa chini ya uangalizi mkali, kwani ndege ya Rais Faustin-Archange Touadéra, iliyokuwa ikirejea kutoka ziarani nje ya nchi, ilikuwa ikisubiriwa kutua kwa wakati wowote.

Idara ya usalama ya Jamhuri ya Afrika ya Kati ilishtushwa na gari la kukodi, lililosajiliwa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati. Kulingana na vyanzo kadhaa, ni gari lililopewa kwa muda kwa Mkuu wa vikosi vya jeshi la Minsuca, kwa kusubiri gari rasmi.

Minusca yasikitishwa na tukio hilo

Katika taarifa, Minusca inasema "inasikitishwa kwa tukio hili" na inalaani "kutumiwa kwenye mitandao ya kijamii". Hakika, picha za Walinda amani wanne waliokamatwa, beji zao za "Umoja wa Mataifa" na zana zao za kijeshi zilisambaa kwenye mitandao ya kijamii jana usiku, kupitia kurasa nyingi barani Afrika. Picha hizo ziliandamana na maoni "Jaribio la kumuua rais wa Jmahuri ya Afrika ya Kati".

Minsuca na Ufaransa wakanusha

Toleo hilo lililochukuliwa na tovuti ya habari inayoaminika kuwa karibu na masilahi ya Urusi nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, lakini likakanushwa na Ubalozi wa Ufaransa na Tume ya Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, Minsuca. Msemaji wa ofisi ya rais, serikali na uongozi mkuu wa polisi wanathibitisha kukamatwa kwa watu hao, lakini wanakataa kuzungumzia kwa sasa shutma dhidi yao. Kulingana na vyanzo kadhaa, watu hao wanne bado wako kizuizini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.