CAR: UN yafanya uchunguzi kuhusu mauaji yanayodaiwa kutekelezwa na vikosi vya jeshi
Umoja wa Mataifa unachunguza mauaji yanayodaiwa kufanywa karibu na mji wa Bria, nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, ambayo yalisabaisha vifo kadhaa wakati wa operesheni ya pamoja ya jeshi la Jmhuri ya Afrika ya Kati na mamluki wa kundi la Wagner kutoka Urusi kuanzia Januari 16 hadi 17, kwa mujibu wa vyanzo vya Umoja wa Mataifa.
Imechapishwa:
Operesheni hii ililenga kundi la wapiganaji la Union for Peace in the Central African Republic (UPC), moja ya vyanzo hivi vimeliambia shirika la habari la AFP kwa sharti la kutotajwa jina.
"Zaidi ya raia 30 waliripotiwa kuuawa, wengine kwa risasi hewa," chama hiki kimeongeza, pia kikibainisha uwezekano wa kuwepo kwa visa vya uporaji ulivyotekelezwa na wahusika wa operesheni hiyo ya kijeshi.