Pata taarifa kuu

UN: Valentine Rugwabiza kushiriki katika kinyang'anyiro cha kuongoza Minusca

Kikosi cha Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, Minusca kinatarajia kuwa na mkuu mpya ifikapo mwisho wa mwezi huu, na mkuu wa Umoja wa Mataifa tayari amewasilisha kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mtaifa mgombea wake, Mnyarwanda Valentine Rugwabiza anatarajia kumrithi Msenegali Mankeur Ndiaye, ambaye amehudumu kwenye nafasi hiyo tangu mwaka 2019.

Mnyarwanda Valentine Rugwabiza anaombwa kuongoza Minusca, kikosi cha Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati. Yeye ni mwanadiplomasia mwenye uzoefu (kwenye picha, mnamo 2010, pamoja na Pascal Lamy, mkurugenzi wa WTO ambaye alikuwa mmoja wa washirika wake wa karibu).
Mnyarwanda Valentine Rugwabiza anaombwa kuongoza Minusca, kikosi cha Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati. Yeye ni mwanadiplomasia mwenye uzoefu (kwenye picha, mnamo 2010, pamoja na Pascal Lamy, mkurugenzi wa WTO ambaye alikuwa mmoja wa washirika wake wa karibu). AFP - GEORGES GOBET
Matangazo ya kibiashara

Hakuna hata mmoja wa wanachama watano wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, ambaye anaweza kushawishi mapendekezo ya Katibu Mkuu, ambaye anayeona tatizo lolote kuhusiana na uteuzi huo.

Wanachama 5 wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa (P5) baada ya kubainisha kwa Jean-Pierre Lacroix kuidhinisha kugombea kwa Valentine Rugwabiza kama mwakilishi wa Katibu Mkuu katika Jamhuri ya Afrika ya Kati, hii inapaswa kuthibitishwa haraka sana na Umoja wa Mataifa.

Balozi wa Rwanda katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa huko New York tangu mwaka 2016, ni mwanadiplomasia wa muda mrefu ambaye Antonio Guterres amemchagua. Ingawa alianza kazi yake katika biashara, aliteuliwa mwaka 2002 kama mwakilishi wa Rwanda katika ofisi ya Umoja wa Mataifa huko Geneva; kisha kutoka mwaka 2005 hadi mwaka 2013, alikuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Biashara Duniani, kabla ya kuchukua nyadhifa za ngazi ya mawaziri huko Kigali. Na kuiwakilisha nchi yake miaka mitatu baadaye huko New York.

Mshirika muhimu wa usalama wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, Rwanda, imekuwa mchangiaji wa kwanza wa wanajeshi katika kikosi cha Umoja wa Mtaifa, Minusca, tangu mwaka huo ikiwa na walinda amani 1,700  kati ya 12,000 walioko nchini Jmjuri ya Afrika ya Kati - wanajeshi wa Rwanda pia wametumwa Bangui katika ngazi ya nchi mbili kutekeleza mkataba wa mwaka 2019. .

Hata hivyo, rais wa Rwanda anasifika kwa kushikamana na suluhu za Kiafrika kwa matatizo ya Afrika, ambayo Valentine Rugwabiza aweza kutafutia ufumbuzi kikamilifu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.