Pata taarifa kuu
DRC-UCHAGUZI

Tume ya Uchaguzi DRC yaomba kuondolewa kwa vikwazo kuhusiana na uchaguzi

Tume ya Uchaguzi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo CENI, imetangaza kuwa Uchaguzi Mkuu ujao utafanyika Desemba mwaka 2023.

Kuna Pia vikwazo vya kiufundi, na vinaweza kuathiri shughuli zetu, lakini pia kuna janga la kiafya la COVID-19, ambalo linaweza kuwa kikwazo kikubwa kwa watu wote. Hizo ndio changamoto kuu ambazo tunapaswa kuzizingatia, ” amesema Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi nchini DRC, Denis Kadima.
Kuna Pia vikwazo vya kiufundi, na vinaweza kuathiri shughuli zetu, lakini pia kuna janga la kiafya la COVID-19, ambalo linaweza kuwa kikwazo kikubwa kwa watu wote. Hizo ndio changamoto kuu ambazo tunapaswa kuzizingatia, ” amesema Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi nchini DRC, Denis Kadima. Caroline Thirion / AFP
Matangazo ya kibiashara

Mwenyekiti wa Tume hiyo Denis Kadima amesema, kalenda hiyo imetolewa kwa kuchelewa kwa miezi 28 na sasa anataka kuondolewa vikwazo vinavyoweza kuathiri kalenda hiyo ya uchaguzi.

 “Tumebainisha vikwazo kadhaa vinavyoweza kuathiri utekelezaji wa muongozo huu wa uchaguzi, kuna vikwazo vya  kisisia ,vya kiusalama, kuna ukosefu wa usalama katika sehemu nyingi za nchi.

Kuna Pia vikwazo vya kiufundi, na vinaweza kuathiri shughuli zetu, lakini pia kuna janga la kiafya la COVID-19, ambalo linaweza kuwa kikwazo kikubwa kwa watu wote. Hizo ndio changamoto kuu ambazo tunapaswa kuzizingatia, ” amesema Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi nchini DRC, Denis Kadima.

Katika hatua nyingine, mjini Goma leo tamasha la nane la kuhimiza amani linafunguliwa na linawakutanisha wanamuziki mbalimbali kutoka nchini humo na kwingineko barani Afrika, kuimba kwa ajili ya amani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.