Pata taarifa kuu
GUINEA-BISSAU-SIASA-USALAMA

Guinea-Bissau: Cipriano Cassama, Kaimu rais, ajiuzulu wadhifa wake

Nchini Guinea-Bissau, Spika wa Bunge la kitaifa, Cipriano Cassama, aliyetawazwa kama rais wa mpito siku ya Ijumaa jioni, ametangaza kwamba anajiuzulu wadhifa wake.

Cipriano Cassama nyumbani kwake huko Bissau akitangaza kujiuzulu kujiuzulu kwenye nafasi yake kama kaimu rais Jumapili, Machi 1, 2020.
Cipriano Cassama nyumbani kwake huko Bissau akitangaza kujiuzulu kujiuzulu kwenye nafasi yake kama kaimu rais Jumapili, Machi 1, 2020. Charlotte Idrac/RFI
Matangazo ya kibiashara

Guinea-Bissau inayoendelea kukumbwa na mgogoro wa baada ya uchaguzi.

Katika taarifa fupi aliyoitoa akiwa nyumbani kwake huko Bissau, akilindwa na askari wa ECOMIB, kikosi cha askari wa Jumuiya ya kiuchumi ya nchi za Afrika ya Magharibi, ECOWAS, na baadhi ya askari wa Guinea, Cipriano Cassama amesema "usalama wangu uko hatarini". Amebaini kwamba Jumamosi jioni, kuna askari walikuja kuwatafuta walinzi wake. Amesema ana hofia usalama wake na wa familia yake.

Amesema pia anataka kuepusha "mapigano kwa maslahi ya taifa na raia wa Guinea-Bissau" na kulaani kitendo cha jeshi kushikilia kwa nguvu makao makuu ya Bunge la taifa.

Cipriano Cassama alitawazwa bungeni siku ya Ijumaa jioni na wabunge 52, hasa kutoka chama cha PAIGC. Kabla ya hotuba yake, Teodora Gomes, mjumbe wa kamati kuu ya chama cha kihistoria, alimwomba asiachii ngazi na asitoe tangazo hilo la kujiuzulu, lakini ameamua kujiuzulu, mashahidi wanasema.

"Nikiangalia vitisho vya kifo vilivyotolewa dhidi yangu, dhidi ya walinzi wangu, naona kwamba usalama wangu uko hatarini. Nimeamua kuchukua uamuzi huu, kuzuia makabiliano kati ya vikosi kutoka upande wa pili na vikosi ambavyo vinanilinda na pia kuzuia vita, sijui kama naweza kuviita vita vya kiraia au umwagaji damu, " amesema Cipriano Cassama.

Kwa hivyo nchi yetu inakabiliwa na mgogoro mpya wa baada ya uchaguzi, mgogoro ambao bado haujatatuliwa kati ya wagombea wawili, Umaro Sissoco Embalo na mpinzani wake, Domingos Simões Pereira, ili tuweze kujua mshindi halali3, ameongeza Bw. Cipriano.

Waziri Mkuu wa Guinea-Bissau Aristides Gomes, ambaye alifutwa kazi na Umaro Sissoco Embalo siku ya Ijumaa, pia amelaani katika mahojiano na RFI vitisho vinavyotolewa, hasa dhidi yake. Ametoa "habari ambayo inaeleza mpango wa kuwaua baadhi ya maafisa ", pamoja na yeye kama Waziri Mkuu.

Waziri Mkuu Aristides Gomes aliyefutwa kazi na Umaro Sissoco Embalo, wakati wa mahojiano na RFI, huko Bissau, Machi 1, 2020
Waziri Mkuu Aristides Gomes aliyefutwa kazi na Umaro Sissoco Embalo, wakati wa mahojiano na RFI, huko Bissau, Machi 1, 2020 RFI/Charlotte Idrac
Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.