Pata taarifa kuu
BURKINA FASO-VIKWAZO

ECOWAS yasitisha uanachama wa Burkina Faso

Mataifa ya Afrika Magharibi yanakutana katika mkutano wa kilele siku ya Ijumaa ili kuamua juu ya vikwazo dhidi ya serikali ya Burkina Faso, ambayo iliingia madarakani katika mapinduzi ya kijeshi siku ya Jumatatu, na ambayo imetoa wito kwa washirika wake wa kimataifa kushirikiana nayo.

ECOWAS, ambayo imetaka kuachiliwa kwa rais aliyepinduliwa Roch Marc Christian Kaboré, aliyewekwa chini ya kifungo cha nyumbani, pamoja na maafisa wengine waliokamatwa, itafanya mkutano mwengine Februari 3 huko Accra.
ECOWAS, ambayo imetaka kuachiliwa kwa rais aliyepinduliwa Roch Marc Christian Kaboré, aliyewekwa chini ya kifungo cha nyumbani, pamoja na maafisa wengine waliokamatwa, itafanya mkutano mwengine Februari 3 huko Accra. © RFI/Serge Daniel
Matangazo ya kibiashara

Burkina Faso imesimamishwa uanachama katika Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Maharibi, bila hata hivyo kutangazwa vikwazo zaidi, kulingana na mshiriki wa mkutano huo.

Burkina Faso, ambako mapinduzi yalifanyika Jumatatu, imeesimamishwa uanachama katika Jumuiya ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS) siku ya Ijumaa kufuatia mkutano wa kilele wa shirika hili ambao bado haujaamua juu ya vikwazo vingine, shirika la habari la AFP limenukuu chanzo kutoka mkutano huo.

ECOWAS, ambayo imetaka kuachiliwa kwa rais aliyepinduliwa Roch Marc Christian Kaboré, aliyewekwa chini ya kifungo cha nyumbani, pamoja na maafisa wengine waliokamatwa, itafanya mkutano mwengine Februari 3 huko Accra, mbele ya wakuu wa nchi kutoka eneo hilo, kulingana na chanzo hiki kikizungumza kwa sharti la kutotajwa jina.

Mali na Guinea, ambako wanajeshi pia walichukua mamlaka, zimechukuliwa vikwazo vipya.

Katika hotuba yake ya kwanza tangu kuchukua mamlaka siku ya Alhamisi jioni, kiongozi mpya wa Burkina Faso, Luteni Kanali Paul-Henri Sandaogo Damiba, kwenye televisheni ya taifa kwamba nchi yake inahitaji washirika wake "zaidi kuliko hapo awali".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.