Pata taarifa kuu
CHAD-MAZUNGUMZO

Chad: Wapiganaji wa makundi yenye silaha na wafungwa wa kisiasa waachiliwa

Ni kipimo cha utulivu kilichoamuliwa na mamlaka ya mpito. Wafungwa hao wameachiliwa huru Jumanne, Januari 18, 2022, kutoka kituo cha kizuizi cha Klessoum karibu na mji mkuu.

Jela kuu la Ndjamena (hapa ilikuwa mwaka 2007) nchini Chad.
Jela kuu la Ndjamena (hapa ilikuwa mwaka 2007) nchini Chad. Getty
Matangazo ya kibiashara

Mamlaka ilikuwa imepitisha sheria ya msamaha mwishoni mwa mwaka uliopita kwa ajili ya watu waliopatikana na hatia ya vitendo vya uasi. Hii ni kuwezesha ushiriki wao katika mazungumzo jumuishi ya kitaifa yaliyotangazwa kufanyika katikati mwa mwezi Februari na ambayo yayafanya iwezekane kuandaliwa kwa mwisho kipindi cha mpito.

Miongoni mwa wafungwa hao, wapiganaji wa makundi yenye silaha, hasa kutoka Muungano wa vikosi vya Upinzani (UFR), ambao walihukumiwa, lakini pia raia wa kawaida walioachiliwa ambao walikuwa wamesalia jela kwa muda mrefu bila kuhukumiwa.

Takriban wapiganaji 300 wa kundi hili la waasi wamenufaika na hatua hii ambayo inalenga kutuliza vurugu, kulingana na Mahamat Ahmat Alhabo, Waziri wa Sheria.

Sheria hii ya msamaha haiwahusu wafungwa wa kivita kutoka kutoka kundi la waasi la Front for Alternation and Change, waliokamatwa baada ya mapigano ya Aprili 2021 ambayo yaligharimu maisha ya rais Idriss Déby Itno, kwa sababu bado hawajahukumiwa. Wanatazamwa na Mkataba wa Geneva, amebainisha waziri wa sheria.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.