Pata taarifa kuu
CHAD-USHIRIKIANO

Chad yatuma wanajeshi 1,000 kuimarisha ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Mali

Mamlaka ya Bamako imekubali kutuma wanajeshi wake 1,000 kushirkiana na ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Mali, na tangazo hilo linakuja wakati maandalizi ya uwepo wa jeshi la Ufaransa nchini Mali yanaendelea.

Mwanajeshi wa Chad kutoka kikosi cha MINUSMA akiwa katika operesheni huko Konna katika eneo la Mopti nchini Mali, Desemba 20, 2018.
Mwanajeshi wa Chad kutoka kikosi cha MINUSMA akiwa katika operesheni huko Konna katika eneo la Mopti nchini Mali, Desemba 20, 2018. MINUSMA/Gema Cortes
Matangazo ya kibiashara

Kikosi cha Chad kinatarajiwa kuongezeka karibu maradufu chini ya mamlaka ya Umoja wa Mataifa. Balozi wa Mali katika Umoja wa Mataifa amethibitisha hilo kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Lakini serikali ya kijeshi iliyoko madarakani huko Bamako imebaini kwamba kutumwa kwa kikosi hiki ni kutokana na makubaliano kati ya nchi hiyo na Chad kwa ombi la serikali ya Jamhuri ya Chad", "kukabiliana na vitisho na kulinda askari wake [...] kaskazini mwa Mali, kufuatia kuondoka kwa kikosi cha Barkhane, "kikosi cha Ufaransa katika ukanda wa Sahel, ambacho kiliwaondoa wanajeshi 450 kutoka kaskazini mwa Mali.

Kwa upande wa Chad, Waziri wa Mambo ya Nje anathibitisha kutumwa kwa wanajeshi 1,000 nchini Mali. Lakini amebaini kwamba haijabainishwa wapi watapelekwa na kwamba maelezo haya yatafafanuliwa kwa makubaliano na Umoja wa Mataifa.

MINUSMA ilikuwa imeamua mwezi Juni kuwaongezea wanajeshi 3,000 katika kikosi chake, katika kukabiliana na kuzuka upya kwa ghasia katikati mwa Mali.

MINUSMA ina wajumbe 16,500 wakiwemo wanajeshi 11,000 kote nchini. Chad imepoteza walinda amani 60 kati ya 159 nchini Mali, wengi wao wakiwa wameuawa katika mashambulizi ya kijihadi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.