Pata taarifa kuu

Mali: Wanasiasa na mashirika wakutana kushutumu muda wa kipindi cha mpito

Jumatano hii, Januari 5, wanasiasa kadhaa na vyama vya kiraia wamekutana katika mji mkuu wa Mali, Bamako, katika makao makuu ya Parena kushutumu ratiba iliyopendekezwa na mamlaka, ambayo inapendekeza muda wa miaka 5 kwa kipindi mpito.

Mji mkuu wa Mali, Bamako, Mei 2, 2016.
Mji mkuu wa Mali, Bamako, Mei 2, 2016. Photothek via Getty Images - Thomas Imo
Matangazo ya kibiashara

Mashirika mengi ya kiraia yalikuwepo katika makao makuu ya Parena kwa wakati huu ambao ulikusudiwa kuwa wa heshima na ambao ulianza kwa dakika moja ya ukimya na kuimbwa kwa wimbo wa taifa, njia ya kuonyesha kuwa hakuna mtu mwenye ukiritimba wa uzalendo katika nchi hiyo.

Wanasiasa na wanaharakati wa mashirika ya kiraia wamekutana ili kushughulikia swali la muda wa kipindi cha mpito, mojawapo ya mapendekezo ya mashauriano ya kitaifa yaliyomalizika hivi karibuni. Kwa upande wa Youssouf Diawara, rais wa muungano wa vyama vya upinzani, amesema kipindi cha mpito kinapaswa kumalizika mnamo Februari 27.

Mkutano wa hadhara pia ulitajwa kufanyika Jumamosi Januari 8 mbele ya mnara wa Mashujaa kutetea kanuni za kidemokrasia. Pia ni njia ya kuonyesha nia ya kuheshimu makataa ya awali ya mpito ya baadhi ya watu wa Mali katika mkesha wa mkutano wa usiokuwa wa kawaida wa Jumuiya ya Nchi za Kiuchumi za Afrika Mgharibi, ECOWAS.

Hapa, wote wanazungumzia hatari za vikwazo kutoka kwa shirika la kikanda na wote wanataka kuviepuka kwa sababu "Mali haina suluhu la kukabiliana na vikwazo".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.